- Delusions, kuona au kusikia vitu ambavyo visivyokuwepo (hallucinations)
- Kukasirika kwa haraka (irritability)
- Inappropiate moods
- Low mood
Viashiria vya general paresis
- Mboni za jicho kuwa katika umbile ambalo si la kawaida
- Mboni kushindwa kupepesuka (changes in pupil response)
- Kupoteza uwezo wa kuhisi mgandamizo au mtikisiko katika ngozi (Loss of sense of vibration or position)
- Kushindwa kusimama wakati mtu amefunga macho (romberg test)
- Kushindwa kutembea vizuri
- Viungo vya mwili kuwa dhoofu
- Matatizo ya kusahau
Vipimo vya uchunguzi
- FTA- ABS – Kipimo cha damu kinachofanya kuangalia antibodies za bakteria aina ya Treponema Pallidum wanaosababisha kaswende
- RPR (Rapid Plasma Reagin) – Kipimo hiki pia huangalia antibodies za Treponema Pallidum katika damu ya wagonjwa wa kaswende
- VDRL (Veneral Disease Research Laboratory)- Kipimo cha kuangalia antibodies za Treponema Pallidum, kipimo hiki kimeshahabiana sana na kipimo cha RPR.
- Lumbar Puncture – Kipimo cha kuchukua maji ya uti wa mgongo ili kuangalia kiwango cha sukari katika maji hayo, presha yake, protini, chembechembe nyekundu na nyeupe za damu, rangi yake, madini ya chloride. Kipimo hiki ni muhimu sana kwani husaidia kutambua kama kuna magonjwa mengine kama ugonjwa wa uti wa mgongo, multiple sclerosis, hypoglycemia, kiharusi, saratani, jipu nk.
- Cranial CT na MRI – CT Scan ya kichwa pamoja na kipimo cha MRI ili kuangalia kama kuna magonjwa mengine mbali na kaswende na kuangalia sehemu ipi ya ubongo iliyoathirika.
- Nerve conduction test – Kipimo cha neva za mwilini
- Vipimo vya macho
Dalili za meningovascular ni
- Mboni kuwa ndogo
- Kupooza kutokana na kuathirika kwa neva mbalimbali
- Kuharibika mishipa ya damu mwilini
- Kupooza upande mmoja wa mwili
- Matatizo ya kumeza chakula – Kumeza chakula kwa shida
- Degedege
- Kupooza neva ya jicho (optic neuropathy)
- Matatizo ya macho (chorioretinitis)
- Ukiziwi
- Vertigo nk.
Vipimo vya uchunguzi vya meningovascular
- Vipimo vya hepatitis
- ELISA for HIV – Kipimo cha ugonjwa wa ukimwi
- PCR (Polymerase Chain Reaction) – Kipimo cha kuangalia vina saba vya bakteria mbalimbali kama Chlamydia trachomatis, Trichomonas vaginalis nk.
- Urinalysis (urine test) – Vipimo vya mkojo
- Tabes Dorsalis husababisha kudhoofika kwa viungo vya mwili kutokana na kuathirika kwa uti wa mgongo pamoja na mishipa ya fahamu. Hali hii ni hatari sana kwani ina kawaida ya kuwa endelevu na huweza kusababisha kifo kwa mgonjwa.
Dalili za Tabes Dorsalis
- Kutembea kwa shida
- Mgonjwa kutembea huku ametanua miguu sana (wide based gait)
- Kudhoofika viungo vya mwili
- Kupoteza uwezo wa kuunganisha hisia na matendo fulani fulani katika mwili (Loss of coordination)
- Kuwa na hisia zisizo za kawaida mwilini kama vile kujihisi vitu vinachoma choma (lightening pains)
- Loss of reflexes
Vipimo vya uchunguzi vya Tabes Dorsalis
- CBC (Complete Blood Count) – Kipimo cha wingi wa damu, kuangalia aina za chembechembe za damu nk.
- Urinalysis – Kipimo cha mkojo
- Lumbar Puncture for CSF – Kipimo cha kuangalia maji ya uti wa mgongo kama nilivyoeleza hapo juu.
- CT Scan – Kipimo cha CT Scan ya kichwa, uti wa mgongo, moyo, mishipa ya damu.
- MRI ya kichwa
- VDRL, RPR, FTS-ABS, MHA-TP – Vipimo vya kuangalia antibodies za bakteria aina ya Treponema Pallidum kama nilivyowahi kueleza.
Tiba ya Neurosyphilis
Tiba ya aina zote za neurosyphilis huusisha kwanza kutibu ugonjwa wa kaswende kwa kutumia dawa za antibiotics aina ya penicillin G au doxycyline kwa wale wanaopata madhara ya penicillin. Hata hivyo kwa wale wenye matatizo na penicillin ni bora kumueleza Daktari mapema ili achukue hatua zinazostahili.
Kwa wale wagonjwa wasioweza kula, kuvaa nguo, wale waliopooza viungo, wasioweza kuzungumza, watahitaji tiba mbalimbali kama rehabilitation therapy, physical therapy, occupation therapy, speech therapy nk.
Dawa za maumivu na degedege zinaweza kutumika kwa wale wenye kupata maumivu na degedege. Kwa wale viziwi, watahitaji vifaa maalum vya kuwasaidia kusikia (hearing aids) baada ya kuonana na Daktari wa masikio, pua na koo.