Image

Matatizo ya Akili (Mental Retardation) - Sehemu ya 2

Katika sehemu ya kwanza ya makala ya upungufu wa akili tuliona makundi ya upungufu wa akili, ukubwa wa tatizo hili, visababishi na pathofiziolojia yake.
 
Sehemu hii ya pili tutaangalia dalili, vipimo vya uchunguzi, tiba yake pamoja na jinsi ya kujikinga na tatizo hili la upungufu wa akili.

Dalili na Viashiria vya Upungufu wa Akili

  • Kuchelewa katika ukuaji wa uwezo wa kuongea/kuzungumza
  • Upungufu wa kumbukumbu (deficits in memory skills)
  • Matatizo katika kufahamu mambo ya kijamii
  • Upungufu wa uwezo wa kutatua matatizo
  • Kuchelewa kukua kwa tabia za vitendo vya kujihudumia mwenyewe (kama kufunga vifungo vya shati nk)
  • Kuendelea kuwa na akili za kitoto
  • Kupungua uwezo wa kusoma
  • Lack of social inhibitors
  • Kushindwa kufikia vigezo vya ukuaji wa kiakili
  • Kushindwa kumudu masomo shuleni
  • Lack of curiosity
  • Utambuzi wa Upungufu wa Akili

    Utambuzi wa upungufu wa akili huusisha
    • Historia ya mgonjwa – Kuhusu mazingira ya sehemu anayoishi, matumizi ya madawa ya aina yoyote, historia ya magonjwa ya akili, tabia ya awali na ya  sasa ya mgonjwa, tiba aliyowahi kupata kuhusu ugonjwa wa akili, jinsi familia na wahudumu ya afya wanavyomchukulia kuhusu hali yake na nk.
    • Vipimo vya afya 
    • Vipimo vya mfumo wa fahamu
    • Mental status examination –Hufanywa na daktari
    • Vipimo vya uchunguzi – Vipimo vya ugonjwa wa kaswende, Rubella, Toxoplasmosis, Cystomegalo virus, Herpes simplex, vipimo vya    mkojo (kuangalia phenylketonuria), kipimo cha EEG kama amewahi kupata degedege, vipimo vya damu na nk.
    • Vipimo vya  saikolojia - The Bayley Scales of Infant Development, The Stanford-Binet Intelligence Scale, The Wechsler Intelligence    Scale for Children-III, and The Wechsler Preschool and Primary Scale of Intelligence-Revised.
    Vigezo vinavyotumiwa na tabibu wa magonjwa ya akili kutambua mgonjwa wa upungufu wa akili kwa watoto {DSM IV (diagnostic and statistical manual) for mental retardation coded on AXIS II (paediatrics)}
    IQ ya 70 au chini yake wakati mgonjwa anafanyiwa kipimo cha akili (IQ test). kwa mtoto mchanga, hupimwa uwezo wa ufanyaji kazi kwa    vipimo vya kliniki (clinical judgement)
    Kutokuwa na uwezo au upungufu katika kujihudumia mahitaji yake  ya kimaisha kutokana na umri wake au utamaduni wake, kuwepo kwa angalau vigezo viwili kati ya hivi basi mgonjwa ndio anatambuliwa kuwa na upungufu wa akilii

    vigezo hivyo ni kama vifuatavyo

    • Kushindwa kuwasiliana na watu, 
    • Kushindwa kujihudumia katika suala zima la usafi, mavazi, chakula (self care) na kushindwa
    • Kuishi nyumbani
    • Kujumuika na watu
    • Kutumia huduma za jamii
    • Kutokuwa na muelekeo (self direction)
    • Kutokuwa na akili darasani au kushindwa kumudu masomo
    • Kushindwa kufanya kazi
    • Kushindwa kustarehe (leisure)
    • Afya (health)
    • Usalama (safety)
    • Kutokea kwa tatizo hili kabla mtu kutimiza  miaka 18

    Tiba ya Upungufu wa Akili

    Tiba ya mtu mwenye upungufu wa akili imegawanyika katika makundi mawili
     
    Huduma za mtu mwenye upungufu wa akili
    • Muathirika kuhudumiwa nyumbani na familia pamoja na familia kupewa elimu ya kijamii ili kuweza kumhudumia
    • Muathirika kuishi katika nyumba za kijamii (foster home) au group home 
    • Rehabilitation centers
    • Asasi za kijamii kusaidia familia ili kuweza kumudu gharama za kumhudumia ndugu au jamaa yao wenye upungufu wa akili.
    • Ushauri nasaha kwa familia ili kuweza kuhimili msongo wa mawazo pamoja na  tabia za mtu mwenye upungufu wa akili
    • Tiba sahihi kwa matatizo ya kisaikolojia pamoja na tabia za mtu wa upungufu wa akili
    • Behavioral modification (using positive and negative reinforcement principle)
    • Matatizo ya kiafya kama degedege yanahitaji tiba sahihi
    • Kumpima uwezo wake wa kiakili mara kwa mara ili kujua ni mahitaji gani  ya shule  muathirika anahitaji. Kupima mara kwa mara ni njia sahihi kwani wengi  hupata nafuu au huonesha maendeleo mazuri na hivyo mahitaji kubadilika kadri muda unavyokwenda

    Tiba yenyewe

    Tiba ya sauti au lugha (speech/language therapy) kutoka kwa madaktari bingwa wa kutibu sauti (Speech/language therapists)

    • Behavioral therapy – Matibabu ya kurekebisha tabia ya muhusika
    • Occupation therapy
    • Huduma za kijamii kwa familia na muhusika
    • Kubadilisha mfumo wa maisha (health lifestyle) kula lishe bora, kufanya mazoezi, kujihudumia, kupunguza msongo wa mawazo kwa wenye upungufu wa akili
    • Ushauri nasaha mara kwa mara au kuhudhuria program maalum za ushauri nasaha na mambo ya kijamii
    • Dawa za ugonjwa wowote wa akili muhusika alionao (antipsychotic medications)
    • Dawa za maumivu kulingana na kiwango cha maumivu
    • Mawasiliano kwa kutumia maandishi, sauti au picha na hata lugha ya vitendo kwa watu wenye upungufu wa akili ili kuleta maelewano wakati wa tiba na kumfanya muathirika kupata hamasa ya kuendelea na tiba
    • Kuwafanyia uchunguzi kama wananyanyaswa kijinsia kama kubakwa nk. Watu wenye upungufu wa akili mara nyingi hubakwa na hivyo kuwafanya kuwa wakali au kuwa na hasira. Daktari anahitajika kugundua anapoona ishara hii kwa mgonjwa wakati wa kumpima.
    • Kuacha kuwanyanyapaa na kuwatenga watu wenye upungufu wa akili

    Je, kinga ya Upungufu wa Akili ni Nini?

    Kinga ya upungufu wa akili imegawanyika katika makundi mawili
     
    Kinga ya awali (Primary Prevention)
    • Kuboresha huduma za afya na kijamii ili kuondoa tatizo la utapia mlo, kuongeza uhamasishaji, kuondoa tatizo la kuzaa watoto njiti, na kutoa elimu kwa kina mama wajawazito juu ya madhara ya madawa ya kulevya, unywaji pombe, magonjwa ya zinaa na nk wakati wa ujauzito
    • Kuboresha huduma za afya za kina mama, tiba ya magonjwa mbalimbali ili kuzuia maambukizi, ajali (trauma), madhara mbalimbali wakati wa ujauzito, kifafa cha mimba, na magonjwa ambayo yanaweza kumuathiri mtoto kabla, wakati na baada ya kuzaliwa.
    • Mtoto kupata chanjo dhidhi ya ugonjwa wa kifua kikuu, ugonjwa wa polio, ugonjwa wa surua na nk.
    • Kuwaelimisha kina mama wajawazito juu ya madhara ya madawa ya kulevya na umuhimu wa kuhudhuria kliniki
    • Kutoa ushauri nasaha kwa wazazi ambao wanaathari za viashiria vya asili (genetic counseling to high risk group)
    • Kufanya tafiti juu ya sababu au vyanzo vya upungufu wa akili pamoja na tiba yake.
    • Kuwaelimisha mama wajawazito jinsi ya kujifungua salama na  umuhimu wa kuwasikiliza wahudumu wa afya wakati wa kujifungua kwani mara nyingi kina mama huwakosesha watoto wao hewa na hivyo kuwaweka katika hatari ya kupata upungufu wa akili na ndio sababu wahudumu wa afya wanakuwa wakali sana kwa kina mama wanaofanya hivyo kuchelea mama asipate mtoto mwenye tatizo hili. Hii itasaidia kuondokana na ile dhana ya kwamba kujifungua hospitali za serikali kwa mama  mjamzito ni adhabu kwani  huwa wanapigwa.
    Kinga ya baadae (Secondary Prevention)
    • Ugunduzi wa mapema na tiba sahihi kwa matatizo yanayoweza kuzuilika kama phenylketonuria, hypothyroidism nk.
    • Ugunduzi wa mapema wa matatizo katika mfumo wa fahamu, mabadiliko ya tabia na hisia ili kukabiliana nayo mapema.
    • Ugunduzi wa magonjwa mbalimbali kama ugonjwa wa kaswende, Rubella nk mapema kabisa ili muathirika apate tiba haraka
    • Kufanya kipimo cha Ultrasound, CT, MRI, mapema ili kuweza kugundua kama mtoto ana kilema chochote katika maumbile, hii itasaidia kupanga na kumhudumia mapema zaidi ili kudhibiti tatizo.
    • Ugunduzi wa upungufu wa akili mapema zaidi kwani kuchelewa kutambua huchelewesha tiba yake.. 
    Mara nyingi watu walio na upungufu wa akili uliopitiliza (profound mental retardation) hufa katika umri mdogo au kabla ya kutimiza miaka 20. Wale wenye upungufu wa akili aina ya mild na moderate, umri wao wa kuishi hupungua sana (reduced life expectancy)
     
    Makala hii imeandikwa kwa msaada wa mtaalamu wa magonjwa ya akili kutoka Mirembe Psychiatry Referral Hospital (Dodoma, Tanzania) anayefanya shahada yake ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
     
     
    Imesomwa mara 6914 Imehaririwa Jumatatu, 05 Novemba 2018 09:26
    Dr Khamis

    Dr. Khamis H.Bakari (MD PhD) ni daktari bingwa,mhadhiri katika chuo cha afya cha Chuo  Kikuu cha Dodoma,mtaalamu wa Tiba na Uchunguzi kwa kutumia mionzi ya nyuklia (Nuclear medicine).

    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.