Kurasa huu unakuwezesha kusoma dalili za magonjwa mbalimbali kulingana na tafiti zilizotolewa na Wizara ya Afya pamoja na Shirika la Afya Duniani. Dalili hizi zitumike kama sehemu kwa ajili ya kukupa ufahamu wa kukuwezesha kuchukua hatua na wala si kwa ajili ya kujitibia. Kumbuka, dalili za magonjwa huweza kuwa kinyume na unavyojisikia (force positive) hivyo ni vipimo pekee ndiyo vinaweza kutoa hitimisho la ugongwa.
Dalili na tabia hatarishi za magonjwa kwa Watu wazima
Fangasi
Dalili za Fangasi
- Kutoka uchafu ukeni kama maziwa ya mgando
- Kufukuta kwenye njia ya mkojo
- Maumivu wakati wa kujaamiiana
- Kuwashwa ukeni nje/ ndani
Visabibishi(Risk factors)
- Kufanya ngono zembe.
- Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.
- Matumizi ya sabuni kwa kunawia sehemu za siri (kwa wanawake).
Fangasi mdomoni/kooni kwenye njia ya chakula
Dalili za Fangasi mdomoni / kooni kwenye njia ya chakula
- Maumivu wakati wa kumeza
- Utando mweupe mdomoni
- Kutapika kila anachokulauu
Visababishi (Risk factors)
- Kuwa mgonjwa wa Kisukari, Saratani au UKIMWI
- Matumizi ya antibayotiki au dawa za stiroidi kwa muda mrefu
- Kufanya ngono ya mdomo
Elimu zaidi juu ya fangasi.
Homa kwa watoto wachanga
Dalili za homa kwa watoto wachanga
- Homa
- Kushindwa kunyoya
- Kulia kupita kiasi
- Kutokuchangamka
Visababishi(Risk factors)
- Kupata maambukizi ya mfumo wa mkojo wakati wa ujauzito.
- Kuishi na ugonjwa wa kisukari.
Elimu zaidi juu ya homa kwa watoto wachanga
Homa ya ini (hepatisis)
Dalili za Homa ya ini (hepatisis)
- Macho kuwa ya njano
- Maumivu ya tumbo upande wa juu kulia
- Kuvimba tumbo
- Homa
- Mwili kuchoka
- Damu kutokuganda kwa haraka
- Uharaka wa Damu kuvilia chini ngozi
Visabibishi(Risk factors)
- Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.
- Kutokunawa mikono mara kwa mara kabla ya kula.
- Kunywa pombe.
- Kuvuta sigara.
- Kuishi na mtu mwenye homa ya ini.
Elimu zaidi juu ya homa ya ini(hepatisis)
Kifua kikuu (TB)
Dalili za kifua kikuu (TB)
- Homa endelevu
- Kukohoa Damu
- Kutokwa na jasho jingi hasa wakati wa usiku
- Kupungua uzito
- Historia ya kuishi na mgojwa wa kifua kikuu
Visababishi (Risk factors)
- Uvutaji wa sigara
- Kuishi katika nyumba isiyo na mzunguko wa kutosha wa hewa
- Kuhudhuria mikusanyiko ya watu wengi
- Kuishi au kumuhudumia mgonjwa wa Kifua Kikuu bila kuchukua tahadhdari
Elimu zaidi kuhusu kifua kikuu(TB).
Kisonono
Dalili za Kisonono
- Kutokwa usaha kwenye uume/uke
- Maumivu ya tumbo chini ya
- Kitovu
- Maumivu wakati wa kukojoa
- Homa
- Kukojoa mara kwa mara
- Maumivu wakati wa kujamiina
- Maumivu/kuvimba korodani
Visababishi (Risk factors)
-
Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja
-
Kufanya ngono zembe
Kaswende
Dalili za Kaswende
- Vidonda kwenye Uume/uke ambavyo haviumi
- Vipele vidogo mwili mzima
- Homa
Visabibishi(Risk factors)
- Kufanya ngono zembe.
- Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.
Elimu zaidi juu ya kaswende.
-
Nephrotic Syndrome.
-
Madhara ya Ugonjwa wa Kaswende katika Mfumo wa Mishipa ya Faham (Neurosyphilis).
-
Magonjwa ya Zinaa - 3: Ugonjwa wa Kaswende
Kisamaki
Dalili za kisamaki
- Kutokwa Uchafu Ukeni wenye harufu kama ya shombo ya samaki.
Visabibishi(Risk factors)
- Kufanya ngono zembe.
- Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.
- Matumizi ya sabuni kwa kunawia sehemu za siri (kwa wanawake).
Kichocho
Dalili za Kichocho
- Maumivu wakati wa kukojoa
- Kutokwa na matonye ya damu mwishoni mwa mkojo
- Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
- Homa
Visabibishi(Risk factors)
- Kuoga au kufanya shughuli za kijamii kwenye mabwawa au maji yaliyotuwama
Elimu zaidi kuhusu kichocho.
Maambukizi katika mfumo wa mkojo (UTI)
Dalili za UTI
- Maumivu wakati wa kukojoa
- Homa endelevu
- Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
- Kuharisha
- Mwili kuchoka
Visababishi (Risk factors)
- Kutozingatia usafi wakati wa haja ndogo / kubwa
- Kujisaidia kwenye choo cha kushare
- Kushiriki mapenzi bila kutumia kinga
- Kutokumaliza dozi ya ugonjwa wa UTI
Elimu zaidi kuhusu UTI.
Malaria
Dalili za malaria
- Homa endelevu
- Kutapika nyongo
- Mwili kuchoka
- Viungo kuuma
- Kukosa hamu ya kula
- Degedege au kukamaa
- Kupoteza fahamu
- Macho kuwa ya njano
- Kuharisha
Visababishi (Risk factors)
- Kuishi sehemu yenye mazalia ya mbu
- Kulala bila kutumia chandarua kilichowekwa dawa
- Kutomaliza dozi ya malaria
Elimu zaidi kuhusu Malaria
Nimonia
Dalili za Nimonia
- Kukohoa Kikohozi kikavu
- Kupumua kwa shida
- Homa
- Kifua kuuma
Visabibishi(Risk factors)
- Ugonjwa wa moyo
Kuhara damu
Dalili za Kuhara damu.
- Mwili kuchoka
- Homa
- Kupika
- Maumivu ya tumbo kwenye kitovu
- Kuharisha kamasi au malendalenda
- Kuharisha damu
Visabibishi(Risk factors)
- Kutokunywa maji safi na salama.
- Kutokua na matumizi sahihi ya choo.
- Kutoku nawa mikono kwa maji tiririka na sabuni (kabla ya kula na baada ya kutoka chooni n.k.
Minyoo
Dalili za Minyoo.
- Maumivu ya tumbo
- Kukosa hamu ya kula
- Kupungua uzito
- Kuwasha sehemu ya haja kumbwa
- Kujisaidia minyoo
- Kuharisha kamasi au malendalenda
Visabibishi(Risk factors)
- Kula nyama isiyoiva vizuri.
- Kula mbogamboga zisizoiva vizuri.
Kuhara maji
Dalili za kuhara maji.
- Maumivu ya tumbo
- Kukosa hamu ya kula
- Kupungua uzito
- Kuwasha sehemu ya haja kumbwa
- Kujisaidia minyoo
- Kuharisha kamasi au malendalenda
Visabibishi(Risk factors)
- Kutokunywa maji safi na salama.
- Kutokua na matumizi sahihi ya choo.
- Kutonawa mikono kwa maji tiririka na sabuni (kabla ya kula na baada ya kutoka chooni n.k.
- Kula chakula kilichoachwa wazi kwa muda mrefu.
Kisukari
Dalili za Kisukari
- Kukojoa mkojo mwingi na mara kwa mara
- Kuhisi kiu kusiko kwa kawaida
- Kula mara kwa mara
- Ganzi ya miguu na mikono
- Kutokuona vizuri
- Kupoteza fahamu
Visabibishi(Risk factors)
- Kuwa na uzito mkubwa au uliopitiliza.
- Kuwa na historia ya mtu mwenye kisukari katika familia.
- Kutofanya mazoezi mara kwa mara.
Elimu zaidi juu ya kisukari.
-
Kisukari (Diabetes Mellitus)
-
Tabibu wa kwanza wa kisukari ni wewe mwenyewe
-
Ugonjwa wa Figo Unaotokana na Kisukari (Diabetic nephropathy)
-
Ishi kwa kujiamini, kisukari sio mwisho wa Maisha
-
Mambo ya kuyaepuka kwa mtu mwenye kisukari
-
Kudhibiti Kisukari wakati wa mfungo wa Ramadhani
-
Jinsi ya kula kwa watu wenye Kisukari
-
Naweza kunywa pombe kama nina ugonjwa wa kisukari?
-
Nafasi ya Tendo la ndoa katika kudhibiti kisukari
-
Upandikizaji wa seli za mfumo wa fahamu waweza kutibu kisukari
Kifafa cha mimba
Dalili za kifafa cha mimba
- Degedege au kukakamaa
- Kutokuona vizuri
- Maumivu kwenye chembe ya moyo
- Kupoteza fahamu
- Maumivu ya kichwa
- Kuchanganyikiwa
- Kuvimba miguu
- kizunguzungu
Visababishi(Risk factors)
- Historia ya shinikizo la damu kwenye jauzito zilizopita.
- Historia ya shinikizo la damu
- Kuishi na ugojwa wa kisukari.
Elimu zaidi juu ya kifafa cha mimba.
Maambukizi katika mfumo wa mkojo (UTI) 0-3YRS
Dalili za maambukizi katika mfumo wa mkojo (UTI) 0-3YRS
- Homa endelevu
- Kuharisha
- Mwili kuchoka
- Kulia wakati wa kukojoa (0-3years)
Visababishi(Risk factors)
- Kuzingatia usafi kwa mtoto mara baada kujisaidia.
Kuharibika mimba chini ya wiki 28 ya ujauzito
Dalili za kuharibika mimba chini ya wiki 28 ya ujauzito
- Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
- Maumivu ya mgongo au kiuno
- Kutokwa na damu au mabonge ya damu ukeni
- Kutokwa na maji ukeni
- homa
Visababishi(Risk factors)
- Kuoga au kufanya shughuli za kijamii kwenye mabwawa au maji yaliyotuwama
- Uvutaji wa sigara uliopitiliza
- Kupata ajali (shambulio la mwili hivi karibuni).
- Kuharibikiwa kwa mimba kwa mwanamke.
Kupasuka kwa chupa ya uzazi chini ya miezi 9 ya ujauzito
Dalili za Kupasuka kwa chupa ya uzazi chini ya miezi 9 ya ujauzito
- Kuvuja maji ukeni hadi kuchuruzika miguuni
- Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
- tumbo la uchungu
- Kuchoka
- homa
- Kutokwa na uchafu ukeni
Visababishi(Risk factors)
- Kubeba ujauzito zaidi ya mara moja.
- Kuwa mwanamke.
- Kunywa pombe.
- Kunavuta sigara.
- Historia kujifungua kabla ya uajauzito kutimia.
- Kuishi na ugonjwa wa kisukari.
- Tatizo la shinikizo la damu
Kutokwa na damu ukeni baada ya miezi 7 ya ujauzito
Dalili za Kutokwa na damu ukeni baada ya miezi 7 ya ujauzito
- Maumivu ya tumbo
- Damu kutoka ukeni
- Mto kuto kucheza kabisa au kutokucheza vizuri
- Mwili kuchoka
- wasiwasi
Visababishi(Risk factors)
- Uvutaji sigara kwa wingi.
- Historia ya shindikizo la damu.
- Ujauzito wa kwanza.
- Kubeba ujauzito zaidi ya mara moja.
- Kutokwa na damu katika ujauzito zilizopita.
Magonjwa ya moyo
Dalili za magonjwa ya moyo
- Kupumua kwa shida ukiwa umelala chali
- Mwili kuchoka kirahisi
- Kukosa hewa wakati umelala usiku
- Kvimba miguu
- Kuhisi moyo kwenda mbio
- Kupoteza fahamu
- Maumivu katikati ya kufua
- Kukohoa kikohozi kikavu
Visabibishi(Risk factors)
- Historia ya magonjwa ya moyo kwenye familia.
- Mgonjwa wa kisukari.
- Unywaji wa pombe kupita kiasi.
- Uvutaji sigara kwa wingi.
- Kuwa na uzito mkubwa au uliopitiliza
Elimu zaidi juu ya magonjwa ya moyo.
-
Unyongovu Waweza Kusababisha Magonjwa ya Moyo kwa Vijana
-
Magonjwa ya Moyo ya Kuzaliwa (Congenital Heart Diseases)
-
Kukakamaa kwa mwili kutokanako na magonjwa ya Moyo
-
Upasuaji wa moyo duniani
-
Maambukizi katika kuta za ndani za moyo (Infective Endocarditis)
-
Athari za madawa ya kulevya kwenye moyo
-
Hatari za kubeba ujauzito kipindi ukiwa na shida ya kufunguka mlango wa kushoto wa moyo
-
Tundu Katika Kuta za Chini za Moyo (Ventricular Septal Defect)
-
Shambulizi la Moyo (Heart Attack)
Maambukizi katika mfuko wa kizazi baada ya kujifungua ndani ya wiki 6 (42 days)
Dalili za Maambukizi katika mfuko wa kizazi baada ya kujifungua ndani ya wiki 6 (42 days)
- Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
- Kutoka uchafu na harufu mbaya ukeni
- homa
- Kukosa hamu ya kula
Visababishi(Risk factors)
- Kujifungua ndani ya wiki sita.
Magonjwa ya figo
Dalili za magonjwa ya figo
- Kuvimba uso haswa wakati wa kuamka asubuhi
- Kuvimba miguu
- Mkojo kuwa na mapovu
- Kuvimba tumbo
- Maumivu kwenye nyonga
- Kwikwi
- Kukosa mkojo kabisa au Kupata mkojo kidogo
Visababishi(Risk factors)
- Kuishi na ugojwa wa kisukari.
- Kunywa pombe kupitiliza.
- Uvutaji wa sigara uliopitiliza.
- Ugonjwa wa moyo.
- Matumizi ya madawa ya kienyeji.
- Matumizi ya dawa za maumivu kwa muda mrefu (mfano apirini na dicklofenaki).
Elimu zaidi juu ya magonjwa ya figo.
Malaria wakati wa ujauzito
Dalili za malaria wakati wa ujauzito
- Homa endelevu
- Kutapika nyongo
- Mwili kuchoka
- Viungo kuuma
- Kukosa hamu ya kula
- Degedege au kukamaa
- Kupoteza fahamu
- manjano
- kuharisha
Visababishi(Risk factors)
- Matumizi ya chandarua chenye dawa.
- Kuishi mazingira yenye mazalia mbu.
Elimu zaidi juu ya malaria wakati wa ujauzito.
Manjano kwa watoto wachanga
Dalili za manjano kwa watoto wachanga
- Macho na au ngozi kuwa ya njano
- Kushindwa kunyoya
- Kutokuchangamka
Visababishi(Risk factors)
- Kupata maambukizi ya mfumo wa mkojo wakati wa ujauzito.
Minyoo
Dalili za minyoo
- Maumivu ya tumbo
- Kukosa hamu ya kula
- Kupungua uzito
- Kuwashwa sehemu ya haja kumbwa
- Kujisaidia minyoo
- Kuharisha kamasi au malendalenda
Visababishi(Risk factors)
- Kula nyama isiyoiva vizuri.
- Kula mbogamboga zisizoiva vizuri.
Maambukizi katika mfumo wa mkojo wakati wa ujauzito
Dalili za maambukizi katika mfumo wa mkojo wakati wa ujauzito
- Maumivu wakati wa kukojoa
- Homa endelevu
- Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
- kuharisha
- Mwili kuchoka
Visababishi(Risk factors)
- Matumizi ya choo cha kukaa.
- Kutokutumia choo ya kisafi.
Pangusa
Dalili za uambukizi kwenye via vya uzazi
- Uvimbe mdogo mwekundu kwenye Uke/Uume wenye maumivu makali.
- Maumivu na Kuvimba korodani.
- Homa.
- Mkojo kuuma au kufukuta wakati wa kukojoa.
Visabibishi(Risk factors)
- Kufanya ngono zembe.
- Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.
Pneumocystis Jirovesi (pcj) protozoa wa mapafu
Dalili za Protozoa wa mapafu(Pcj)
- Kukohoa Kikohozi kikavu
- Kuhemea jujuu
- Mwili Kuchoka
- Kupungua uzito
- Kutetemeka
Visababishi (Risk factors)
- Upungufu wa kinga mwilini.
Shindikizo la damu (presha)
Dalili za shindikizo la damu (presha)
- Kichwa kuuma upande
- Kuhisi mapigo wa moyo kwenda mbio
- Ganzi miguni na mikono
- Kutokuona vizuri
Visabibishi(Risk factors)
- Unywaji wa pombe uliopitiliza.
- Uvutaji wa sigara kwa wingi.
- Kuwa na uzito uliopitiliza au mkubwa sana.
- Kuishi na ugonjwa wa kisukari.
- Kutofanya mazoezi mara kwa mara.
Elimu zaidi juu ya shindikizo la damu
Seli Mundu (sickle cell)
Dalili za Seli Mundu (sickle cell)
- Maumivu au kuvimba maungio ya mwili.
Visababishi(Risk factors)
- Historia ya seli mundu kwenye familia.
- Kuoa au kuolewa mtu mwenye vinasaba na wewe(ndugu).
Upungufu wa damu
Dalili za Upungufu wa damu
- Mwili kuchoka sana
- Kizunguzungu
- Kupumua kwa shida
- Kupoteza fahamu
- Kichwa kuuma chote
- Kuvimba miguu
- Kuhisi moyo kwenda mbio
Visabibishi(Risk factors)
- Ugonjwa wa seli mundu.
- Mgonjwa mwenye maradhi haya; Kisukari, saratani, vvu/ukimwi kifua kikuu, magojwa ya moyo na magojwa ya figo
Elimu zaidi juu ya upungufu wa damu.
Utapia mlo
Dalili za utapia mlo.
- Kupungua au kuongezeka uzito
- Kukosa hamu ya kula
- Kusinyaa kwa ngozi
- Nywele kabadilika rangi na kuwa kama za mzee
- Kuvimba miguu
- Kutokuchangamka
- Kuvimba tumbo.
Visababishi(Risk factors)
- Kutokula mlo kamili.
- Kunyonyesha mtoto kwa mda mrefu pasipo kumpatia chakula kengine.
- Mtoto kuwa na magonjwa sugu kama ugonjwa wa moyo au upungufu wa akili.
Upungufu wa damu wakati wa ujauzito
Dalili za Upungufu wa damu wakati wa ujauzito
- Mwili kuchoka sana
- kizunguzungu
- Kupumua kwa shida
- Kupoteza fahamu
- Kichwa kuuma chote
- Kuvimba miguu
- Kuhisi moyo kwenda mbio
Visababishi(Risk factors)
- Mgonjwa wa seli mundu.
- Kula mlo kamili mlo kamili .
- Kusumbuliwa na ugonjwa wowote kati ya haya kisukari, saratani, na vvu/ukimwi.
Elimu zaidi juu ya upungufu wa damu.
Upungufu wa damu (watoto)
Dalili za Upungufu wa damu (watoto)
- Mwili kuchoka sana
- Kizunguzungu
- Kupumua kwa shida
- Kupoteza fahamu
Visababishi(Risk factors)
- Historia ya seli mundu kwenye familia.
- Unaumwa ugonjwa wowote kati ya haya, Kisukari, Saratani,vvu/ukimwi.
- Unakula mlo kamili.
Viashiria vya awali vya mimba
Dalili za awali za mimba
- Kutopata hedhi
- Homa za asubuhi na jioni
- Kichefuchefu na au kutapika
- Tumbo kuuma chini ya kitovu
- Maumivu ya titi
- Kuongezeka kwa titi
- Kuongezeka au kupanda kwa mstari mweusi kwenye tumbo la mwanamke.
Visababishi(Risk factors)
- kuwa mwanamke
- kushiriki tendo la ndoa bila kutumia kinga
- Kubalehe
Viambukizi kwenye via vya uzazi
Dalili za uambukizi kwenye via vya uzazi
- Maumivu wakati wa kujaamiiana.
- Kutoka uchafu Ukeni.
- Kutokwa damu ukeni kusiko eleweka.
- Historia ya kujifingua au kuharibika kwa mimba.
- Maumivu ya tumbo chini ya kitovu.
- Homa.
- Kusikia baridi na kutetemeka.
Visabibishi(Risk factors)
- Kufanya ngono zembe.
- Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.
- Matumizi ya sabuni kwa kunawia sehemu za siri (kwa wanawake).
VVU (Ukimwi)
Dalili za virusi vya ukimwi(VVU)
- Kifua kikuu
- Kuhara sugu
- Utando mweupe mdomoni
- Kuvimba matezi mwilini
- Upele/Ukurutu
- Mkanda wa Jeshi
- Maumivu makali ya kichwa
- Kupungua Uzito sana
- saratani ya Ngozi
Visababishi (Risk factors)
- Kutofanyiwa tohara kwa mwanaume.
- Kushiriki ngono zaidi ya mtu mmoja.
- Kushiriki ngono bila kinga(ngono isiyo salama) mwenza usiejua hali yake.
- Kushiriki ngono bila kinga na mwenza mwenye maambukizi ya vvu.
- Kushiriki ngono kinyume na maumbile.
- Kushiriki ngono ukiwa umelewa.
- Matumizi ya dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga.
- Matumizi ya vitu vyenye ncha kali (mfano kiwembe, sindano nk).
- Kupata ajali na watu zaidi ya wawili na kugusana damu za majeraha.
- Kushiriki biashara ya ngono ( Kudanga).
- Kuugua magonjwa ya zinaa (mfano kisonono, kaswende, n,k).
- Kushiriki ngono ya mdomo.
Elimu zaidi juu ya Vvu/Ukimwi.
-
Mambo ya kuzingatia unapogundulika kuwa na maambuki ya virusi vya ukimwi.
-
Matumizi Sahihi na Utaratibu wa Kuanza Dawa za Kufubaza Makali ya Virusi vya Ukimwi - ARV
-
Imani potofu kuhusiana na VVU/Ukimwi
-
Dalili za ugonjwa wa Ukimwi na jinsi ya kujikinga
-
Jinsi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU)
Vidonda vya tumbo
Dalili za vidonda vya tumbo
- Maumivu ya kwenye chembe ya moyo
- Kutapika damu
- Maumivu ya tumbo wakati wa kula / wakati wa njaa
- Kiungulia
- Kubeuwa
- Maumivu wakati wa kumeza
- Kupata choo kama lami
Visabibishi(Risk factors)
- Matumizi vya ya vyakula vyenye viungo vingi kupitiliza (spicies) .
- Matumizi ya dawa za maumivu kwa muda mrefu mfano apirini na dicklofenaki.