Image

Homa ya kweli inasababisha wasiwasi hasa katika miezi michache ya kwanza ya maisha ya mtoto. Hii ni kwa sababu mfumo wa kinga kwa watoto huwa bado mchanga na hauna ufanisi sana katika kupambana na maambukizi kwa miezi mitatu au minne ya mwanzo baada ya mtoto kuzaliwa.

Hivyo ni muhimu kujifunza namna sahihi ipasayo kuchukua joto la mtoto wako na kuelewa nini kinaashiria homa ya kweli.

Homa kwa mtoto

Kwa kawaida madaktari husema mtoto ana homa iwapo kama joto la mwili wake litaongezeka na kufikia nyuzijoto >37.5?? (99.5F) au zaidi. Ni vizuri kujua joto la kawaida la mtoto wako kwa kuchukua vipimo mara chache wakati mtoto yupo katika hali ya kawaida ‘mzima wa afya’.

Nini husababisha homa kwa watoto?

Kuna sababu kadhaa ziletazo homa kwa watoto. Upungufu wa maji mwilini ni mojawapo ya sababu hizo. Aidha joto la watoto wachanga linaweza kuwa juu kufuatia nguo nyingi alizovaa katika mazingira ya joto kiasi. Kwa kawaida inashauriwa mtoto wako avae safu moja zaidi ya mavazi zaidi ya yale ambayo wewe mwenyewe ukivaa yanakufanya ujisikie vizuri, maana yake ni kwamba kama wewe umevaa nguo mbili juu, na ukajisikia vema, basi mtoto wako avae walau nguo tatu ili kulinda joto lake lisipungue wala kuongezeka sana.

Sababu nyingine iwezayo kuleta homa kwa watoto ni maambukizi. Mfumo wa kinga ya mwili wa mtoto unapohisi kuingiliwa na vimelea vya maradhi kama vile bacteria au virusi, hutoa taarifa kwenye ubongo ambao nao hutoa kemikali fulani zinazosababisha joto kupanda mwilini. Kupanda kwa joto huko ambako huitwa homa kunaweza kuwa na faida kadhaa katika mwilini wa mtoto zikiwemo;

  • Baadhi ya bakteria na virusi hawapendi hali ya joto la juu na hivyo basi ni rahisi zaidi kuharibiwa na mfumo wa kinga.
  • Joto la juu la mwili husaidia mwili kupambana na maambukizi.

Kucheua kwa mtoto ni hali ya mtoto kutoa chakula kupitia mdomoni muda mfupi baada ya kula/kunyonya.Kucheua kwa mtoto hupungua kadri mtoto anavyokuwa mkubwa na ni nadra sana kutokea baada ya mtoto kufikisha umri wa miezi 18.

Kucheua pia kunaweza kuashiria tatizo kubwa zaidi kwa mtoto kama ugonjwa wa Gastro-esophageal Reflux Disease (GERD), mzio (allergy) au kuziba kwa mrija wa kupitishia chakula.

Nini husababisha mtoto kucheua baada ya kula? 

  • Utafiti mpya unaonesha ya kwamba watoto wanaokunywa juisi au ambao mama zao walikunywa vitu vyenye sukari kipindi cha ujauzito wapo kwenye hatari kubwa ya kuugua ugonjwa wa Pumu
  • Wajawazito ambao walikunywa soda na vinywaji vyenye sukari (sugary beverages) wana asilimia 70 ya kuzaa watoto ambao baadae watapata ugonjwa wa Pumu

Matokeo ya utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani yameonyesha ya kwamba, watoto wanaokunywa vinywaji vyenye sukari au juisi (artificial juice) na ambao mama zao walikunywa soda kipindi cha ujauzito wao wapo kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa Pumu.

Watoto ambao waligundulika kuwa na kiwango kikubwa cha sukari aina ya fructose (ambayo hupatikana kwenye juisi au soda) kwenye milo yao kipindi cha ukuaji, walikuwa kwenye hatari ya asilimia 79 kupata ugonjwa wa Pumu ukilinganisha na watoto ambao hunywa vinywaji vyenye sukari kwa nadra au wale watoto ambao hawanywi kabisa vinywaji hivyo.

Kina mama ambao walitumia vinywaji vyenye sukari au soda kipindi cha ujauzito pia walikuwa kwenye hatari ya asilimia 70 kuzaa mtoto ambae baadae atagundulika kuwa na ugonjwa wa Pumu ikilinganishwa na kina mama ambao walitumia vinywaji vyenye sukari kwa nadra au ambao hawakutumia kabisa vinywaji hivyo kipindi cha ujauzito.

Kichwa maji au hydrocephalus (kwa lugha ya  kitaalamu) ni mkusanyiko usio wa kawaida wa maji yanayojulikana kitaalamu kama (cerebral spinal fluid) kwenye ventrikali (ventricles) au nafasi zilizo wazi (cavities) kwenye ubongo. Tafiti zinaonyesha kuenea (prevalence) kwa kichwa maji  duniani ni; kwa kila watu 100,000 basi watu 85 wana tatizo la kichwa maji na hii inatofautiana kulingana na umri.

 kwa watoto;kati ya watoto 100,000 watoto 88 wana tatizo kichwa maji.

Hali hii huweza kusababisha kuongezeka kwa shinikizo katika fuvu (increased intracranial pressure).  Hydrocephalus limetokana na lugha ya kigiriki ambalo humaanisha: Hudro - Maji , na Kephalos - Kichwa

Kwa kawaida kwa kila mtu huwa na maji yanayoitwa kitaalamu cerebral spinal fluid kifupi CSF ambayo huzunguka ndani ya ventrikali za ubongo, nje na ndani ya ubongo na kuelekea kwenye uti wa mgongo (spinal cord) ambapo hufyonzwa na kurudi kwenye damu. Kichwa maji husababishwa na uzuiwaji wa mzunguko wa CSF, au kufyonzwa kwake au uzalishwaji wa CSF kwa wingi kupita kiasi kama kwenye papilloma of choroid plexus. Ikumbukwe ya kwamba kichwa maji huweza hata kusababisha kifo.

Kuna aina mbili za kichwa maji ambazo ni

Communicating hydrocephalus (Non obstructive hydrocephalus)

Aina hii husababishwa na kutokufyonzwa kwa maji ya CSF ingawa hakuna uzuiwaji wake wa mzunguko baina ya ventrikali na nafasi iliyopo kwenye ubongo inayojulikana kama Subarachnoid space. Hii inaweza kuleta madhara kama uvujaji wa damu baina ya ventrikali au kwenye Subarachnoid space, ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis) nk. Aina hii ya kichwa maji nayo imegawanyika katika sehemu mbili, ambazo ni

  • Normal Pressure Hydrocephalus (NPH) – Katika aina hii ventrikali za kwenye ubongo zimeongezeka ukubwa na kuongeza pressure ya CSF.
  • Hydrocephalus ex vacuo – Katika aina hii, pia kuna kuongezeka ukubwa kwa vetrikali za ubongo na subarachnoid space kutokana na kusinyaa kwa ubongo ambapo kunaweza kusababishwa na ugonjwa wa dementia, baada ya kupata ajali ya kichwa au matatizo ya akili kama Schizophrenia.

Non communicating hydrocephalus (Obstructive hydrocephalus)

Aina hii husababishwa na uzuiwaji wa mzunguko wa CSF kwenda kwenye Subarachnoid space kutokana na uvimbe wa kwenye ventrikali.
Kwa hiyo mtu anaweza kuwa na kichwa maji kutokana na kuzaliwa nacho (congenital) au akakipata baadae maishani (acquired) baada ya kupata maradhi kwenye mfumo wa neva mwilini (CNS infections), ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis), uvimbe kwenye ubongo, ajali ya kichwa, kuvuja damu kwenye ventrikali nk. Kichwa maji anachopata mtu baadae maishani huwa kinaambatana na maumivu makali sana.

Kwa nini watoto wachanga wanalia?

Ni kawaida kwa watoto kulia. Hata watoto wanaozaliwa na afya njema kabisa wanaweza kulia kwa jumla ya wastani wa kati ya saa moja mpaka matatu kwa siku. Kwa vile watoto hawawezi kujifanyia chochote wao wenyewe zaidi ya kutegemea wazazi, walezi ama watu wengine wanaowazunguka katika kuwapatia chakula, joto, na faraja, kilio ni njia ya mtoto ya kuwasilisha moja ya mahitaji hayo.

Kama mzazi mpya, wakati mwingine inakuwa vigumu kutambua mtoto wako anahitaji nini anapolia. Mzazi anaweza kuwa na maswali kadhaa kichwani mwake, je, mtoto ana njaa, anasikia baridi, ana kiu, anaumwa ama amechoka? Katika siku za mwanzo, hali ya namna hii inawawia vigumu wazazi wengi, wasijue nini la kufanya. Hata hivyo, kwa kadiri siku zinavyopita mzazi mpya ataweza kutambua kuwa kilio cha mtoto wake kinamaanisha anahitaji nini kutokana na mfumo wake wa kulia.