Image
×

Onyo

JUser: :_load: Haiwezi kupakia mtumiaji aliye na kitambulisho: 797

Assalamu’alaikum Warahmutullahi Wabarakatuh. Natumai mu wazima wa afya na mnaendelea vyema na majukumu ya kila siku.

Waumini wa dini ya Kiislam duniani kote wameingia katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Hivyo,katika muendelezo wa makala zinazohusu kisukari, tunaoenda tujikumbushe au tujifunze mambo machache ya kufanya kabla, wakati na baada ya kipindi takatifu cha mfungo wa Ramadhani.

Tukiwa tuna amini kuwa watu wengi wanaoishi na tatizo la Kisukari hasa aina ya pili ya kisukari wanatamani sana kufunga Ramadhani katika kutimiza moja ya nguzo za imani ya dini ya Kiislam, na kwa imani Funga ni dawa kiroho na kimwili pia.

Jambo la kwanza kwa mtu mwenye kisukari ni kujiweka tayari kwa funga miezi mitatu au minne kabla, kuitayarisha akili na nafsi,hii itakusaidia kuwa mwangalifu sana katika ulaji wako na mfumo mzima wa ulaji.

Kufanya kipimo cha hba1c ni muhimu kwa sababu inaonesha kiwango cha sukari miezi mitatu na hii inakufanya ujue kama utaweza kufunga ramadhan bila kuwa tatizo lolote au hutaweza kufunga. Kupima sukari kabla na baada ya kula kabla ya mfungo wa ramadhani pia ni muhimu,kabla ya kula ni lazima sukari iwe chini ya sita(6) na masaa mawili baada ya kula iwe chini ya nane (8) na kama majibu yatakuwa hivyo kila mara hii itakuonesha kuwa unaweza kufunga bila tatizo.

Jambo la pili ni kuhakikisha unapata ushauri kutoka kwaa daktari wako wa kisukari, Shauriana naye, usiamue kufunga Ramadhani bila ya kushauriana na daktari wako, hii ni muhimu kwa sababu anaweza kukupa ushauri kulingana na kiwango chako cha sukari kwa miezi mitatu nyuma.(hba1c) na kipimo cha sukari cha kila siku unachopima kabla na masaa mawili baada ya kula.

Wakati wa mfungo ni lazima mtu mwenye kisukari atambue kuwa anaweza kufunga baada ya ushauri na ruhusa dakitari wake,na endapo akifunga, ni lazima pia awe anapima kiwango cha sukar kabla ya kuanza ,mfungo,kwa mfano, kabla ya kula daku ni lazima apima,hii itamsaidia kujua kama ataweza kufunga kwa siku hiyo ama Lah, kama akipima na kiwango cha sukari kikiwa sita (6) au saba(7) anaweza kufunga lakini indapo akipima akikuta kwango cha sukar iki chini ya sita (6), labda ni tano(5) au nne (4) hatoweza kufunga kwa sababu moja ya kisababisho cha sukari kushuka ni kukaa bila kula kwa muda mrefu.

U-hali gani msomaji wetu wa makala zetu za kisukari, karibuni tena katika makala nyingine ya kisukari, leo tunaangalia kwa ufupi tu  siku na mwezi ya kisukari duniani, na pia tutadadavua kwanini kuna mwezi wa kisukari na malengo yake hasa ni nini na pia kwa kuwa sio wote wananojua kuhusu mwezi wa kisukari, karibuni.

Kila mwaka ifikapo mwezi wa November ni siku ya kisukari duniani, mwezi huu wote umetengwa kuwa ni mwezi maalum kwa kueleza elimu na uelewa juu ya tatizo hili ya kisukari, pia kuboresha matibabu ya maradhi yanayotokana na kisukari, maadhimisho wake ni tarehe kumi na nne (14) ya mwezi November.

Kwanini iwe mwezi wa November, tarehe kumi na nne(14)? Inawezekana unajiuliza hili swali kila mara na kila ifikapo mwezi November, shirika ya afya duniani na shirikisho ya kimataifa la kisukari yalikutana na kukubalia kutenga tarehe kumi na nne (14)  November  kuwa ni mwezi wa kisukari duniani kwa sababu ni mwezi ambayo  ndugu Frederick Banting ambaye ni mgunduzi wa kichocheo kiitwacho INSULIN ambacho hutumika kama dawa kwa wengi aina ya kwanza ya kisukari alizaliwa. Katika kumuenzi mgunduzi huyu mashirika haya mawili wakaona ni busara kutenga mwezi huu na tarehe hii kuwa ni siku ya kisukari duniani kote.

Tafiti iliyofanywa na Chama cha Kisukari Tanzania mwaka 1999, ilionesha kuwa maradhi yasiyo ya kuambukiza (maradhi ya moyo,figo,saratani, kisukari na mengineyo yasiyo ya kuambukiza) huchangia karibu asilimia 60 ya vifo vyote duniani na asilimia 43 ya ukubwa wa tatizo la maradhi hayo kote duniani.Maradhi haya yasiyo ya kuambukiza yanaongezeka na kukua kwa kasi hasa katika nchi zinazoendelea ikiwepo Tanzania. Tanzania inakisiwa kuwa ifikapo mwaka 2020 maradhi haya yatasababisha asilimia 73 ya vifo vyote duniani na ukubwa wa tatizo litaongezeka mpaka asilimia 60. (Tanzania Diabetes Association. 2013)

Kwa aina ya kwanza ya kisukari,ambayo hii huwapata watoto kwenye umri wa mwaka 1-25 inazidi kuongezeka katika nchi nyingi duniani,baadhi ya tafiti zilizowahi kufanywa zinaonesha katika watoto 79,000 ambayo wapo chini ya umri wa miaka 15 wapo katika hatari ya kupata tatizo la aina ya kwanza ya kisukari duniani kote,aina hii ya kwanza sio kama aina ya pili,aina ya ya kwanza,hasababishwi na mfumo wa maisha, au uzito uliopitiliza, na pia aina ya kwanza haiwezi kuzuilika tofauti na aina ya pili ya kisukari.inakadiriwa kuwa takriban 497,000 ya watoto wanaishi na aina ya kwanza ya kisukari duniani kote na pia nusu ya idadi hiyo ya watoto wanaishi katika mazingira magumu hasa kimatibabu na dawa.(International Diabetes Federation, IDF Diabetes Atlas.2014)

Watu takriban milioni 371 wamepata  kisukari kote duniani,ikiwa asilimia 80 ya idadi hiyo wanaishi katika nchi zenye uchumu wa kati na nchi masikini.katika tanzania, inasemekana kuwa katika watu 9 kwa kila watu 100 ya watanzania wenye umri wa miaka 25 na kuendelea wana tatizo la kisukari na pia katika idadi hiyo ya watu 9 ni wawili tu wanajijua kuwa wana tatizo la kisukari.(Tanzania Diabetes Association. 2013)

Namba, idadi na takwimu zinaonesha dhahiri shahiri ni kiasi gani kisukari ni tatizo kubwa endapo tu kama jamii haitapewa elimu ya kutosha kuhusu tatizo hili, jamii pia ni lazima ijue kwa upana na undani zaidi kuhusu chanzo,dalili na jinsi ya kuepuka na kuishi na kisukari.tatizo hili la kisukari mara nyingi napenda kusema sio ugonjwa ila inakuwa ni ugonjwa endapo tu mtu hatakuwa makini katika kudhibiti kiwango cha sukari.

Bado tupo katika mwendelezo wa Makala yetu kuhusu kisukari na jinsi ya kuishi na kisukari. Katika makala ya kwanza katika mfululizo huu wa makala za kisukari, Ishi kwa kujiamini, kisukari sio mwisho wa Maishatulianza kwa kuangazia jinsi ya kuishi na kisukari, pia mambo makuu manne ya kuzingatia kwa wagonjwa wenye kisukari.

Baada ya kupata ufahamu juu ya umuhimu wa kujiamini kwa mtu anayeishi na kisukari,katika makala ya Jinsi ya kula kwa watu wenye Kisukari, tuliangazia  suala la jinsi ya kula, maana hapo ndipo tatizo lilipo, watu wengi wenye tatizo la kisukari hawafahamu ni aina gani ya vyakula wanapaswa kula na wengine wanaingia kwenye gharama kubwa kununua vyakula tofauti wakiamini kuwa ni maalum kwa wenye kisukari.

Leo tunaangalia suala zima la udhibiti wa kisukari kwa mtu mwenye kisukari. Lazima ufahamu kuwa wewe mwenye kisukari ni Tabibu wa kwanza wa tatizo lako. Kuna matatibu wengi sana mitaani na wote wana utaalamu tofauti,pia kuna taarifa nyingi mitaani na  kwenye mtandao ila ni jukumu lako wewe kujua ni taarifa gani sahihi na inayokufaa.

Unaweza kuambiwa kula aina hii ya chakula, usile aina ile ya chakula,acha kabisa kula aina hii ya chakula,kula sana aina ile ya chakula, mara kula sana aina hii ya matunda,usile aina ile ya matunda. Kwa mfano, wengi wanaambiwa wale ndizi changa kwa wingi,labda na ugali wa uwele,dona au ulezi kwa wingi. Sasa mathalani, umeenda sehemu ambapo hakuna ndizi changa,hakuna dona,ulezi au uwele, unataka kusema hautakula chakula? Utashinda na njaa? La Hasha, utakula tu, mwenye kisukari anakula  aina zote za chakula, iwe wali,ndizi za kupika,pilau,biryani,viazi vya aina yote, maboga,sembe,dona n.k, cha msingi ni kujua ni jinsi gani au kwa utaratibu gani unaweza kula vyakula hivyo.

Tusipikiwe au tusitengewe chakula tofauti na cha familia, hapana, tunakosea sana, chakula cha familia  ndio na wewe  mwenye ugonjwa wa kisukari unaweza kula chakula hicho hicho, hakuna chakula maalum cha mtu mwenye kisukari,isipokuwa tu wewe mwenyewe ni lazima ufahamu ni jinsi gani unatakiwa ule au ni kwa utaratibu gani unatakiwa ule, ndio maana ninasema wewe mwenye kisukari ndiyo tabibu wa kwanza wa kisukari.mimi nitakushauri,mpishi atapika tu na chakula kitawekwa mizani, ila wewe ndiyo utajua jinsi ya kula.Wewe ni Tabibu wa kwanza wa kisukari chako.

Miongoni mwa magonjwa sugu yanayoendelea kuathiri afya za mamilioni ya watu wa nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania ni ugonjwa wa kisukari. Ugonjwa huu hutokea pale ambapo tezi kongosho linaposhindwa kutengeneza kichocheo aina ya Insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho cha insulin na kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha sukari kwenye damu au hyperglycemia.

Aina za Kisukari

Kisukari kimeanishwa katika makundi yafuatayo

Aina ya kwanza ya Kisukari au Type 1 Diabetes Mellitus

Hii ni aina ya kisukari inayowaathiri zaidi watoto na vijana (young adults).

Aina hii hutokea iwapo seli maalum zinazotengeneza homoni ya insulin zijulikanazo kama beta cells of Islet of Langerhans katika tezi kongosho zitakosekana au zitaharibika kwa sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.

Moja ya madhara ya ugonjwa wa kisukari katika mwili wa binadamu ni ugonjwa wa figo (diabetic nephropathy). Ugonjwa huu ambao huwapata watu wenye kisukari, hutokea muda mrefu baada ya mtu kugunduliwa kuwa na kisukari.

Kinachotokea (Pathofiziolojia)

Figo zinaundwa na mamia kwa maelfu ya vijiumbo vidogo vidogo viitwavyo nefroni (nephrons). Kazi ya hizi nefroni ni kuchuja damu na kutoa uchafu mwilini mwako kwa njia ya mkojo.

Kwa watu wenye kisukari, nefroni huwa na tabia ya kukakamaa, kuzeeka na kuwa na makovu kadiri miaka inavyopita. Baada ya muda fulani, hushindwa kabisa kazi yake ya kuchuja uchafu, matokeo yake protini ambazo kwa kawaida huwa haziwezi kuchujwa, huchujwa na kutoka katika mkojo.

Chanzo hasa cha kuzeeka, kukamaa na kuwa makovu huku kwa nefroni hakijulikani. Hata hivyo inadhaniwa kuwa uthibiti mbaya wa sukari husababisha uharibifu wa figo, na madhara huongezeka maradufu kwa watu wenye shinikizo la damu lisilothibitiwa na kisukari kwa pamoja.

Karibuni tena katika kijiwe chetu,leo kwenye muendelezo wa makala zetu kuhusu udhibiti wa kisukari  tunaangalia umuhimu wa tendo la ndoa katika kusaidia kupunguza kiwango cha juu ya sukari.

Kwa upande moja ama mwingine tendo la ndoa ni moja ya zoezi la mwili kama mazoezi mengine kama kukimbia na mazoezi mengine ya viungo na pia tendo hili linasaidia sana kushuka kiwango cha sukari, Moja ya tafiti iliyowahi kufanya na  American Journal of Medicine inasema kuwa mtu akifanya tendo la ndoa mara tatu au nne kwa wiki anajiweka kwenye nafasi ya kutopata matatizo ya msongo wa mawazo ambayo unaweza kuleta matatizo kama ya Kisukari na Presha.

 Moja ya tafiti iliyofanywa na Taasisi ya Kisukari Marekani (ADA) zinaonesha kuwa kufanya tendo la ndoa husaidia kuyeyusha mafuta na sukari mwilini kwakuwa ni moja ya mazoezi ya viungo.Tafiti zingine zinaonesha kuwa endapo mtu ukifanya tendo la ndoa mara tatu au nne kwa siku husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini.

Habari! Karibuni tena katika muendelezo wa makala zetu kuhusu Kisukari ambazo zinapatika katika tovuti pendwa ya TANZMED, Mara ya mwisho tulikumbushana kuwa wewe ndio tabibu ama daktari wa tatizo lako, wewe sio mgonjwa wewe ni mtu wenye kisukari, ama una ishi na kisukari, ni kitu cha kawaida sana kwa dunia ya sasa.

Sasa leo napenda kuwakumbusha ni vitu gani au ni mambo gani mtu wenye kisukari anatakiwa kuviepuka. Kama tujuavyo kuwa endapo Kisukari haitadhibitiwa ipasavyo basi inaweza kuleta madhara mengi kama kupata kiarusi,upofu, matatizo ya moyo, vidonda ndugu,matatizo ya figo na ini,kwa wanaume kukosa nguvu vya kiume, matatizo ya misuli na kadhalika. Sasa kwa sisi wenye kisukari tuishi vipi ama tufanye nini ili kuepuka haya yote?

  1. Jambo la kwanza ambalo mara nyingi napenda kuwakumbusha watu watu wenye kisukari kuwa ni muhimu sana kujikubali, hili ni jambo ya kwanza kwakuwa ukijikubali kuwa una tatizo la kisukari inakuwa rahisi sana kubadili mfumo wa maisha uliyokuwa unaishi kabla ya kupata tatizo  na mara nyingi nasisitiza umuhimu wa kumpatia ushauri nasaha kwa watu wenye kisukari.
  2. Jambo la pili ni kuepuka kabisa na kupunguza kutumia vitu ama vyakula vinavyoweza kupandisha sukari yako kwa haraka,vitu kama soda,juisi,keki,sukari,asali, Chokoleti na vitu vya kupunguza hasa hasa ni vyakula vya wanga na matunda,hapa nikisema matunda simaanishi kuwa matunda walisiwe hapana,ninachomaanisha hapa ni liliwe tunda na sio matunda na kwa muda, ima masaa mawili au lisaa limoja baada ya chakula.
  3. Jambo la tatu ni kuepuka kupata vidonda kwa kuwa kama hujaweza kudhibiti kisukari ni rahisi sana kidonda kuchelewa kupona kwa hiyo basi yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ya kuizngatia;
  • Epuka kutembea bila viatu,yaani kutembea peku, kwa maana unaweza kujikata na kitu chenye ncha kali kama sindano, chumba, miiba nk
  • Epuka kutumia vitu vyenye ncha kali kutaka kucha kwa mfano usitumia wembe au mkasi kukata kucha ili kuepuka kupataka na kupata kidonda,pendelea sana kutumia nail taker.
  • Epuka kuvaa viatu na soksi za kubana, na pia hakikisha miguu yako ni mikavu kila muda, kwa hiyo basi utokapo kuoga ama kunawa miguu, hakikisha unaikausha vizuri hasa katikati ya vidole, kwa sababu kama ukiacha unyevunyevu ni rahisi kutengeneza lengelenge na pia endapo utapata lengelenge usitumbue, acha na likaule lenyewe
  • Kwa wanawake, epuka kuvaa viatu virefu kwa sababu vinazuia damu kufanya mvunguko wake wa kawaida (blood circulation)

Kwa kumalizia napenda kusisitiza tu kuwa kisukari sio mwisho wa maisha,na pia kumbuka kuwa watu wenye kisukari ni watu wanaoishi katika mfumo sahihi wa maisha.

Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa tishio sana hasa kwa wale wanaougua ugonjwa huu kutokana kuwa na athari nyingi sana kama mgonjwa kupata kiharusi, kupoteza viungo mbalimbali  vya mwili kama vile kukatwa mguu/miguu, kidole/vidole na hata kupoteza uwezo wa kuona (diabetes retinopathy), na athari hizi hutokea endapo ugonjwa  wa kisukari haujadhibitwa vyema.

Ugonjwa huu wa kisukari unaweza usiwe ugonjwa  wa kutisha endapo tu mwenye kisukari ataweza kuishi kwa kujiamini na kujikubali, wataalam wanasema kuwa mtu kuishi na ugonjwa  huu wa kisukari anahitaji mambo makuu manne :-

Kujikubali

 Kujikubali ni jambo  muhimu sana, kutayarisha akili yako na kuikubali hali hiyo ya kuwa na  ugonjwa wa kisukari,na kuiambia akili yako kuwa ugonjwa huu hauponi ni hali ambayo itakuwepo katika umri wa maisha yako yote na kuwa tayari kubadili mfumo wako mzima wa maisha.Hii ni sawa na mtu aliyezaliwa upya.

Kubadili mfumo wa Ulaji

Ukijikubali kuwa una  ugonjwa wa kisukari ni rahisi sana kubadili mfumo wako mzima wa ulaji, hii inamaanisha kuwa mfumo wako wa ulaji unaweza kusababisha kupanda kwa sukari (glucose level) au kushuka kwa sukari. Ulaji wa vyakula vya wanga kwa wingi husababisha sukari kupanda. Kuacha kabisa ulaji na matumizi ya vitu ama vyakula vyenye sukari, kwa mfano soda, keki, barafu za sukari (ice cream), chokoleti n.k.

Pia kupunguza matumizi ya mafuta wakati wa uandaaji  wa chakula na kuacha matumizi ya vyakula vyenye mafuta mengi kwa mafano ulaji wa viazi vya kukaanga (chips), maandazi, vitumbua, n.k. Ulaji wa mboga za majani/salad/kachumbari kwa wingi ni muhimu sana. Sahani ya chakula itawaliwe na mboga za majani,na hii ni kwa kila mlo yaani chakula cha asubuhi,mchana na cha jioni.

Mazoezi ya Viungo

Mazoezi ni muhimu kwa afya, mazoezi huchangamsha mwili,hupunguza mapigo wa moyo na kuyafanya kuwa ya wastani pamoja na kuongeza mzunguko wa damu kwa mtu wenye ugonjwa kisukari (hivyo hupunguza hatari ya kupoteza kiungo cha mwili kwa mgonjwa wa kisukari kutokana kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vyake), mazoezi yana nafasi kubwa sana kwa sababu husaidia kuyeyusha lehemu (cholesterol)  mwilini na kuondosha hatari ya kupata tatizo la kiharusi (stroke). Mazoezi yanayohitajika hapa ni yale ya kuchoma mafuta na sio ya kupanua misuli, mazoezi hayo ni kama kukimbia, kuruka kamba,kuogelea,kutembea kwa mwendo kasi. Mazoezi haya yafanyike kwa muda wa nusu saa au saa moja kila siku asubuhi au jioni.

Ugonjwa wa kisukari ni tatizo ambalo siku hizi husababishwa na mfumo wa maisha tunayoishi hasa vijana, tafiti zilizowahi kufanywa zinaonesha kuwa vijana wapo kwenye hatari kubwa ya kupata kisukari kwa sababu ya mfumo usio sahihi wa maisha wanayoishi vijana.

Kutokufanya mazoezi, kukosa muda wa kupumzika na kutokula mlo sahihi,unywaji wa pombe na uvutaji sigara wa kupitiliza, hizi ni sababu chache zinazochangia vijana kuishi katika mfumo wa maisha hatarishi wa kupata maradhi ya kisukari.

Leo tunaangalia suala zima la chakula kwa watu mwenye maradhi ya kisukari,madaktari wapo wengi sana kwenye hospitali zetu pamoja na majumbani mwetu lakini wewe mwenye ugonjwa wa  kisukari ndiyo daktari namba moja katika kutibu afya yako.

Kitu muhimu kwa mgonjwa wa kisukari ni  kufahamu ya kwamba  ana uwanja mpana  sana wa vyakula anavyoruhusiwa kula tofauti na  na mazoea yaliyojengeka miongoni mwetu kuwa mtu anayeuugua maradhi haya basi ana  vyakula vyake vya kipekee kabisa. Maisha ya mtu mwenye kisukari yanatakiwa kuendelea kama kawaida, na unaruhusiwa kula aina zote za vyakula isipokuwa tu vile venye sukari.