Mwezi na siku ya kisukari duniani kwa mara ya kwanza ilizinduliwa na kuadhimishwa mwaka 1991,uzinduzi na maadhimisho hayo yalifanywa chini ya shirikisho la kimatatifa ya kisukari(IDF),baada ya hapo ndipo shirika ya afya duniani wakaitambua mwezi wa November kama ni mwezi wa kisukari duniani na maadhimisho ni tarehe 14.
Tangia hapo mpaka leo dunia inakumbuka na kuadhimisha siku hii ya kisukari duniani, na kila mwaka kunakuwa na kaulimbiu tofautitofauti, kauli mbiu ya mwaka huu kimataifa inahusu na imegusa moja kwa moja wanawake, “WANAWAKE NA KISUKARI” hii ni kwa sababu wanawake ni moja wa wahanga wakuu katika kupata tatizo hili, kuna aina ya tatu ya Kisukari, aina hii ya kisukari huwapata wanawake wajawazito na pia aina hii ya kisukari ni moja ya sababu kuu za vifo vya mama na mtoto.
Kwa Tanzania bado kuna changamoto nyingi katika kupambana na kuzuia uongezeko la tatizo hili ya kisukari, moja ya changamoto kuu ni ukosefu wa elimu na uelewa juu ya tatizo hili ya kisukari, katika watu kumi(10) ni wawili tu wenye uelewa na elimu sahihi ya kisukari,wengi wetu hatujui dalili za kisukari, sababu zinapelekea mtu kupata kisukari. Elimu inahitajika kwa kiasi kikubwa na elimu hii isitolewe tu kila siku na mwezi wa kisukari, kila siku kila miezi iwe ni siku ya kisukari,elimu itolewe kuanzia mashuleni,majumbani na sehemu zingine .kwa pamoja tunaweza kupunguza ongezeko ya idadi ya watu wenge kisukari.