Tafiti iliyofanywa na Chama cha Kisukari Tanzania mwaka 1999, ilionesha kuwa maradhi yasiyo ya kuambukiza (maradhi ya moyo,figo,saratani, kisukari na mengineyo yasiyo ya kuambukiza) huchangia karibu asilimia 60 ya vifo vyote duniani na asilimia 43 ya ukubwa wa tatizo la maradhi hayo kote duniani.Maradhi haya yasiyo ya kuambukiza yanaongezeka na kukua kwa kasi hasa katika nchi zinazoendelea ikiwepo Tanzania. Tanzania inakisiwa kuwa ifikapo mwaka 2020 maradhi haya yatasababisha asilimia 73 ya vifo vyote duniani na ukubwa wa tatizo litaongezeka mpaka asilimia 60. (Tanzania Diabetes Association. 2013)
Kwa aina ya kwanza ya kisukari,ambayo hii huwapata watoto kwenye umri wa mwaka 1-25 inazidi kuongezeka katika nchi nyingi duniani,baadhi ya tafiti zilizowahi kufanywa zinaonesha katika watoto 79,000 ambayo wapo chini ya umri wa miaka 15 wapo katika hatari ya kupata tatizo la aina ya kwanza ya kisukari duniani kote,aina hii ya kwanza sio kama aina ya pili,aina ya ya kwanza,hasababishwi na mfumo wa maisha, au uzito uliopitiliza, na pia aina ya kwanza haiwezi kuzuilika tofauti na aina ya pili ya kisukari.inakadiriwa kuwa takriban 497,000 ya watoto wanaishi na aina ya kwanza ya kisukari duniani kote na pia nusu ya idadi hiyo ya watoto wanaishi katika mazingira magumu hasa kimatibabu na dawa.(International Diabetes Federation, IDF Diabetes Atlas.2014)
Watu takriban milioni 371 wamepata kisukari kote duniani,ikiwa asilimia 80 ya idadi hiyo wanaishi katika nchi zenye uchumu wa kati na nchi masikini.katika tanzania, inasemekana kuwa katika watu 9 kwa kila watu 100 ya watanzania wenye umri wa miaka 25 na kuendelea wana tatizo la kisukari na pia katika idadi hiyo ya watu 9 ni wawili tu wanajijua kuwa wana tatizo la kisukari.(Tanzania Diabetes Association. 2013)
Namba, idadi na takwimu zinaonesha dhahiri shahiri ni kiasi gani kisukari ni tatizo kubwa endapo tu kama jamii haitapewa elimu ya kutosha kuhusu tatizo hili, jamii pia ni lazima ijue kwa upana na undani zaidi kuhusu chanzo,dalili na jinsi ya kuepuka na kuishi na kisukari.tatizo hili la kisukari mara nyingi napenda kusema sio ugonjwa ila inakuwa ni ugonjwa endapo tu mtu hatakuwa makini katika kudhibiti kiwango cha sukari.
Kama kisukari hakijadhibitiwa ipasavyo,ni rahisi kwa mtu mwenye kisukari kupata maradhi yafuatayo:-
- Maradhi ya moyo
- Shinikizo ya damu na kiharusi
- Matatizo ya mishipa ya damu na fahamu,vidonda visivyopona
- Maradhi ya figo,macho
- Kupungua au kuisha kabisa kwa nguvu za kiume.
Jamii inahitaji kujua kuwa tatizo hili ya kisukari ni rahisi sana kuepukika hasa kwa aina ya pili ya kisukari, ili kuepuka kupata aina hii ya pili ni lazima jamii ifanya mambo yafuatayo:-
- Kubadili mfumo mzima wa ulaji, (kula mlo uliyokamilika,makundi matatu muhimu ya chakula,mboga za majani,protini na wanga, kupunguza matumizi ya mafuta ya kula,kupunguza kula protini aina ya nyama nyama kwa wingi,kupunguza kula chumvi nyingi na vyakula vya sukari)
- Kula kwa wingi vyakula vyenye asili ya nyuzinyuzi/mizizi(mihogo,magimbi,viazi.maboga,dona na ngano isiyokobolewa)
- Kuwa na mazoezi ya kula matunda na mboga za majani kwa wingi
- Kufanya mazoezi,(kutembea,kukimbia,kuruka kamba,kuendesha baiskeli,michezo mbalimbali kama mpira)
Endapo jamii itaweza kubadilika na kuishi hivyo basi itasaidia kwa kiasi fulani kupata maradhi ya kisukari,mara nyingi napenda sema kuwa kudhibiti kisukari ni rahisi sana na wala haigharimu uhai wako zaidi ya kuishi katika misingi sahihi ya ulaji unaofaa.ni heri tuzibe nyufa kuliko kuchelewa na kupata gharama za kujenga ukuta,matibabu ya maradhi yanasababishwa na kisukari ni gharama sana kulinganisha na maisha ya mtanzania wa hali ya kati na ya chini.