MAHITAJI
120 gram mbegu za alizeti au unaweza tumia mbegu za ufuta
1 Boga dogo, menya, toa mbegu na katakata vipande
1 kitunguu kikubwa kilichokatwa katwa
5 gram kitunguu thomu
1 karoti kubwa, kata kata vipande vya ukubwa kama kwenye picha
240 gram paneel cheese au unaweza tumia ( mushrooms/uyoga )
1 kijiko kikubwa cha chakula korosho za kuoka zilizokatwa katwa
1 fungu la corriender na parsley kwajili ya kupambia
5 gram chuvi
5 gram pilipili manga
Muda wa Kuandaa:Dakika 30
Jinsi ya kuandaa fuatilia picha na maelezo hapa chini

Weka maboga katika baking pan, nyunyizia mafuta kiasi pamoja na pilipili manga

Roast katika oven kwa moto wa 400F(204.4C) kwa muda wa dakika 20 hadi 30 hakikisha inaiva na ukibonyeza inabonyezeka yaani laini wastani.

Kisha weka mafuta katika kikaango na kikishapata moto weka kitunguu, karoti na paneel cheese pamoja na chumvi na kitunguu thomu endelea kukaanga.

Kisha weka maboga yaliookwa kwenye oven pamoja na mbegu za ufuta au mbegu za alizeti pia unaweza tumia hata mbegu za maboga endelea kukaanga na onja kama chumvi au pilipli manga haitoshi ongezea kiasi.

Kisha mwagia kwa juu majani ya korrienda na parsley kuongeza ladha na kuongeza rangi katika muonekano wa chakula chako.

Chakula hiki ni safi sana kwa afya ya mlaji kwani hakina mafuta kabisa pia ni tajiri sana kwa virutubisho, kumbuka kumwagia kwa juu zile korosho za kuokwa kabla ya kumpatia mlaji.

Chakula hiki unaweza kula kama kilivyo au ukaongeza nyama, samaki, chapati au mkate na ukafurahia mlo huu wewe na familia yako.
NI RAHISI SANA KUANDAA NA HAKINA GHARAMA KABISA WAANDALIE FAMILIA YAKO CHAKULA BORA NA WEWE