Image

Kuosha uso mara kwa mara hukufanya uonekane mzee

kuosha-uso

Siku hizi watu wengi wanapenda kuonekana vijana, kuanzia kwa watu mashuhuri hadi kwa watu wasio mashuhuri, hakuna mtu anayetaka kuzeeka. Tafiti zinaonesha kuwa kuna baadhi ya matendo ambayo waweza kufanya au kuyaepuka huweza kukusaidia kupunguza au kukufanya uonekana mzee kabla ya muda.

Baadhi ya matendo yanayoweza kukufanya usionekane mzee harraka ni kama; kulala chali, kula kwa wingi samaki wa jamii ya salmoni, kujiupusha na mionzi ya moja kwa moja ya jua, kutovuta sigara na mengineyo. Lakini je unafahamu kuwa kuosha sana sura yako hukufanya uonekane mzee?

 Tafiti zinaeleza kuwa, maji huondoa unyevunyevu (moisture) na mafuta ya asili yanayoilinda ngozi ya sura na mikunjo inayokufanya uonekane mzee. Hivyo, kuosha uso mara kwa mara pia huosha unyevunyevu huu.Hivyo unashauriwa kuwa kama una ulazima wa kuosha sura mara kwa mara, basi tumia sabuni zilizo na unyevu (moisturizers)

Imesomwa mara 3868 Imehaririwa Jumatatu, 25 Juni 2018 16:31
Mkata Nyoni

Mkata Nyoni ni mtaalamu wa masuala ya Uchumi na Biashara ya Teknohama. (Information Economics & IT Management). Ni muanzilishi na mkurugenzi wa kampuni ya Dudumizi Technologies LTD inayojishughulisha na masuala yautengenezaji wa Website, Web Systems na Applications za simu.

https://www.dudumizi.com | Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Makala shabihana