Mimba inayotishia kutoka (threatened Abortion)
Tatizo hili hutokea mapema wakati wa ujauzito. Hali hii hujionesha kwa damu kutoka ukeni wakati njia ya shingo ya uzazi ikiwa bado imefunga. Mara nyingi mimba inayotishia kutoka haina tabia ya kuambatana na maumivu yeyote ya tumbo.
Daktari anapompima mgonjwa hukuta shingo ya kizazi ikiwa imefunga na hakuna dalili zozote za kiumbe kutoka ingawa mgonjwa hutokwa na damu sehemu za siri. Aidha mgonjwa huwa hana maumivu yeyote ya tumbo.
Mimba isiyoepukika kutoka (inevitable abortion)
Hii ni hali inayotokea mapema wakati wa ujauzito pale damu inapotoka ukeni wakati njia ya shingo ya kizazi ikiwa imefunguka au kuwa wazi. Aidha, kwa kawaida, kiasi cha damu kinachotoka ni kingi na mgonjwa hujisikia maumivu makali sana ya tumbo.
Utokaji mimba usioepukika waweza kupelekea
- Utokaji mimba ulio kamili (.co.tzplete abortion) au,
- Utokaji mimba usio kamili (in.co.tzplete abortion).
Utokaji mimba usio kamili (in.co.tzplete abortion)
Utokaji mimba usio kamili huambatana na utokaji damu kwa wingi sehemu za siri za mgonjwa, kufunguka kwa njia ya shingo ya kizazi, kutoka kwa baadhi ya mabaki ya kiumbe (products of conception) ingawa mengine hubakia, na mgonjwa kujisikia maumivu makali ya tumbo hususani sehemu za chini ya kitovu.
Utokaji wa mimba ulio kamili (.co.tzplete abortion)
Hali hii huambatana na mama kutokwa damu sehemu za siri, kujisikia maumivu makali ya tumbo pamoja na kutoka kwa kiumbe ikiambatana na kondo lake la nyuma. Aidha baada ya muda, mgonjwa hueleza kupotea kwa maumivu ya tumbo, damu kupungua kutoka sehemu za siri na kufunga kwa njia ya njia ya shingo ya kizazi (cervix).
Mimba iliyotoka bila kugundulika kuwa imetoka (missed abortion)
Hali hii hutokea pale ambapo, kiumbe kinapokuwa kimekufa bila ya mimba kutoka. Mara nyingi, damu huwa haitoki sehemu za siri, na mgonjwa huwa hajisikii maumivu yeyote ya tumbo. Aidha huwa hakuna dalili zozote za ukuaji wa mimba na hata mapigo ya moyo ya mtoto hayawezi kutambulika hata kama vipimo maalum vitatumika.
Utokaji wa mimba unaojirudia rudia (recurrent abortion)
Hali hii hutokea pale ambapo mama huwa na historia ya mimba kutoka mara tatu au zaidi kwa mfululizo.
Utoaji mimba kinyume cha sheria (illegal abortion)
Utoaji mimba kinyume cha sheria ni usitishwaji wa maisha ya mimba au kutolewa kwa kiumbe kinyume na sheria za nchi husika zinavyoagiza. Katika mazingira kama haya, sababu dhahiri za kitaalamu hukosekana isipokuwa wahusika hutenda kulingana na sababu zao binafsi zikiwemo za kutoitaka mimba au kama ni muhusika ni mwanafunzi huogopa kufukuzwa shule.
Utoaji mimba kisheria kwa sababu za kitabibu (therapeutic abortion)
Utoaji mimba ulioidhinishwa kitabibu ni usitishwaji wa mimba kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama. Usitishwaji huu ni hufanywa kitaalamu na daktari. Sababu zinazoweza kufanya mimba ikasitishwa ni pamoja na
- iwapo kiumbe kina mapungufu mengi ya kimaumbile (fetal anomally) ambayo yatamletea mtoto atakayezaliwa matatizo na hata kusababisha kifo chake
- iwapo mama mjamzito alipata ujauzito kwa kubakwa na asingependa kuzaa, au
- iwapo mama mjamzito ana kansa , kwa mfano, kansa ya kiwanda cha mayai ya kike (ovarian cancer), kansa ya damu (leukemia) au kansa ya tezi la goita (thyroid cancer)
Mambo gani hufanya mimba kutoka kwa hiyari?
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kupelekea mimba kutoka kwa hiyari (spontaneous abortion). Miongoni mwa sababu hizo ni
- Matatizo kwenye mfumo wa jenetiki (genetic abnormalities) ambayo husababisha kuharibika na kutoka kwa mimba katika miezi mitatu ya mwanzoni.
- Matatizo kwenye mfuko wa uzazi (uterine problems): matatizo kama vile kuwepo kwa uvimbe kwenye mfuko wa uzazi wa mwanamke (uterine fibroids), au kulegea kwa milango ya shingo ya kizazi (cervical in.co.tzpetence) husababisha mimba kutoka katika theluthi ya pili ya ujauzito (second trimester).
- Sababu nyingine ni pamoja na maradhi wakati wa ujauzito kama malaria, kisukari, shinikizo la damu, kifafa cha mimba, matatizo kwenye tezi ya 'goita' (hypothyroidism). Aidha maambukizi kama Rubella, toxoplasmosis na mengineyo nayo pia huweza kusababisha mimba kutoka.
- Kukosekana kwa ulinganifu katika baadhi ya homoni mwilini (hormonal imbalance)
- Matumizi ya baadhi madawa kwa mfano zinazotumika katika kutibu msongo wa mawazo kama vile paroxetine au venlafaxine nayo yaweza kusababisha utokaji wa mimba.
Tabia hatarishi zinazoweza kusababisha utokaji wa mimba
- Unywaji pombe uliopitiliza.
- Uvutaji sigara
- Utumiaji madawa ya kulevya kama vile kokeini (cocaine)
- Utumiaji kwa wingi wa vinywaji vyenye kiasili cha caffeine kama vile kahawa au kakao.
Vipimo na Uchunguzi
Ili kutambua kuwepo kwa hali hii ya mimba kutoka, vipimo vifuatavyo vyaweza kufanywa na tabibu
- Kipimo cha mimba kwa kutumia mkojo (Urine for hCG)
- Kupima damu ili kufahamu kiasi cha wingi wa damu (haemoglobin level), kundi la damu (blood group) na muda wa damu kuganda (bleeding and clotting time).
- Kuchunguza iwapo shingo ya uzazi imefunga au ipo wazi, na pia kuchunguza iwapo kuna dalili ya kiumbe kutoka ama la. Uchunguzi huu huitwa speculum examination.
- Ultrasound ya nyonga (pelvic utrasound) kwa ajili ya kutambua iwapo kiumbe kipo ama la, na kama kipo je ki hai ama kimekufa.
- Aidha ni muhimu pia kufanya uchunguzi wa magonjwa mbali ya zinaa ambayo husababisha mimba kutoka.
Matibabu ya utokaji wa mimba
Matibabu ya utokaji wa mimba hutegea sana aina ya utokaji wa mimba. Hata hivyo, ni muhimu kuzingatia vitu vifuatavyo wakati wa kutoa matibabu kwa mtu aliyepoteza mimba
Wahudumu wa afya huzingatia kanuni zote (ABC) za kuokoa maisha ya mgonjwa kama vile
- kuhakikisha njia ya hewa ya mgonjwa ipo wazi na hewa inaingia na kutoka vizuri kwenye mapafu
- kuhakikisha mgonjwa anapumua vizuri bila shida
- kuhakikisha mishipa ya damu ya mgonjwa imewekwa mrija wa veni (intravenous line) na mgonjwa anapewa dripu ya maji ya normal saline.
- kuhakikisha mgonjwa anaongezwa damu haraka iwapo vipimo vitaonesha kuwa alipoteza damu kwa wingi
Matibabu ya mimba inayotishia kutoka (threatened abortion)
Kwenye hali hii, mgonjwa hutakiwa
- kupumzika kitandani bila kufanya kazi yeyote (.co.tzplete bed rest) angalau kwa wiki moja au zaidi mpaka hapo damu itakapoacha kabisa kutoka
- kumpa ushauri na uhakika mama ili kumfanya atulie kiakili (assurance and proper councelling)
- Mama pia hupewa dawa za kumtuliza na kumfanya apumzike (sedatives) kama vile phernobabitone
- Aidha mama hupewa dawa kwa ajili ya kupunguza kusukuma kwa uterus (antispamodics) kama vile salbutamol
- Kutofanya tendo la ndoa kwa wiki mbili au tatu
- Aidha mama na mumewe hupewa ushauri juu ya tatizo hilo na jinsi ya kuendelea na matibabu
Matibabu ya mimba iliyotoka kamili (.co.tzplete abortion)
Mara nyingi mgonjwa huwa haitaji matibabu zaidi ya uangalizi wa karibu kwa vile kiumbe pamoja na kondo lake la nyuma vyote huwa vimetoka kikamilifu. Mara chache sana, kulingana na jinsi daktari atakavyoona, mgonjwa anaweza kupewa antibiotiki kwa ajili ya kuzuia uwezekano wa kupata maambukizi.
Matibabu ya utokaji wa mimba usiokuwa kamili (in.co.tzplete abortion)
Matibabu ya aina hii ya utokaji wa mimba uhitaji mgonjwa kusafishwa kwa ajili ya kuondoa mabaki ya kiumbe (products of conception) yaliyobakia. Usafishaji huu huweza kufanywa kwa kutumia njia inayoitwa Manual Vacuum Aspiration (MVA).
Aidha mgonjwa hupewa dawa za antibiotiki kwa ajili ya kuzuia uwezekano wa maambukizi ya vimelea vya bakteria.
Matibabu mimba iliyotoka bila kugundulika kuwa imetoka (missed abortion)
Matibabu ya aina hii ya utokaji wa mimba ni pamoja na mgonjwa kuwekewa maji ya uchungu ili kiumbe kiweze kutoka. Wakati mwingine, daktari anaweza kuamua kusafisha mfuko wa uzazi (uterus) kwa kutumia njia inayoitwa dilatation and curettage. Sambamba na matibabu hayo, mgonjwa pia hupewa dawa za antibiotiki kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya vimelea vya bakteria.
Matibabu ya tatizo la utokaji wa mimba unaojirudia (recurrent abortion)
Jambo la msingi katika matibabu ya tatizo la utokaji mimba unaojirudia (recurrent abortion) ni kugundua na kutambua chanzo kinachosababisha tatizo hilo na kisha kukishughulikia ili kuondoa kabisa kujirudia rudia kwa tatizo hili.