Utangulizi:
Mara nyingi tumeona katika mitandao ya kijamii au katika story za vijiweni tunasikia maambukizi ya njia ya mkojo(UTI) yakihusishwa na magonjwa ya zinaa. Je swala hili lina ukweli ndani yake? Katika makala hii tutaenda kuona maana ya maambukizi ya njia ya mkojo, aina zake, visababishi na tabia hatarishi, dalili, matibabu na tutajibu swali letu lililohamasisha Makala hii.
STI ni nini?
Magonjwa ya zinaa (sexually transmitted infections) ni maambukizi yanayosababishwa na vijidudu kama bacteria,virusi, n.k ambavyo vinaenezwa kwa njia ya ngono. Maambukizi haya huweza kushambulia maeneo tofauti ya mwili ikiwemo mfumo wa uzazi, mfumo wa mkojo, ngozi, macho,mdomo, na hata ubongo.
UTI ni nini?
UTI (Urinary Track Infection) ni maambukizi ya mfumo wa mkojo ambayo mara nyingi husababishwa na bacteria wanaopatikana kwenye mfumo wa chakula (mfano E.choli) au fangasi. Bacteria hawa kupitia vichochezi mbalimbali hupata upenyo wa kuingia kwenye Mrija wa mkojo ambao husafirisha mkojo kutoka kwenye kibofu hadi nje ya mwili (urethra). Kutoka hatua hii maambukizi haya huendelea kushambulia mwili kwa kupanda kufuata njia ya mkojo hadi kufika kwenye figo. Kutokana na kupanda huku kwa mashambulizi haya tunaweza kugawanya UTI katika makundi matatu:
- Urethritis : maambukizi kwenye urethra
- Cystitis : maambukizi kwenye kibofu cha mkojo
- Pyelonephritis: maambukizi kwenye figo
Vichochezi/visababishi hataraishi vya UTI
1. Jinsia (Maumbile)
50-60% ya wanawake wote hupata maambumbukizi ya mfumo wa mkojo angalau mara moja katika maisha yao. (Medina, 2019, #)
Wanaume pia hupata maambukizi ya mfumo wa mkojo lakini Idadi hii kwa wanaume ni ndogo zaidi kulinganisha na wanawake kwasababu ya tofauti katika maumbile ya mfumo wa mkojo. Uwezekano huongezeka kwa wanaume ambao hawajatairiwa.Wanaume wasiotahiriwa ni asilimia 32%, ikilinganishwa na asilimia 8.8% kwa wanaume waliotahiriwa. (Morris & Krieger, 2018, #)
Njia ya mkojo ya mwanamke (urethra) ni fupi kuliko ya mwanaume na hufanya mashambulizi ya vijidudu kupanda kwa haraka zaidi. Lakini pia njia ya mkojo (urethra) ya mwanamke ipo karibu na maumbile ya nje ya mfumo wa uzazi na njia ya haja kubwa, hii husababisha wadudu kuweza kuhama kiurahisi na kushambulia njia ya mkojo.
2. Usafi duni
- Kutokuwa msafi au kujisafisha vizuri katika eneo la haja kubwa na uke kunaweka mazingira rafiki ya vijidudu kuzaliana kwa kasi na kuweza kuhama kiurahisi kuingia kwenye njia ya mkojo. (namna sahihi ya kujisafisha ni kutoka mbele kurudi nyuma)
- Kutokujikausha vizuri baada ya kujisaidia na kuvaa nguo zinazobana muda wote kunatengeneza mazingira rafiki kwa vijidudu hivyo kuzaliana kwani vijidudu hivyo hupenda mazingira ya joto na yenye ubichi/unyevu.
- Kutokujisafisha vizuri baada ya tendo la ndoa. Hii husaidia kusogeza vijidudu karibu na njia ya mkojo.
3. Kutokunywa maji ya kutosha
kutokunywa maji ya kutosha kunasababisha kukojoa mara chache kwa siku na hivyo mkojoo hukaa mda mrefu kwenye kibofu, hali hii hutengeneza mazaliano mazuri ya vijidudu.
4. Kukaa mda mrefu bila kukojoa
kukaa kwa mkojo kwa mda mrefu kwenye kibofu hutengeneza mazingira rafiki kwa vijidudu kuzakliana. Kukojoa mara kwa mara kunaweza kusaidia kusukuma vijidudu kutoka kwenye mfumo wa mkojo.
Umri
kwa jinsia ya kike UTI hushamiri zaidi kwa watoto. Hii ni kwasababu ya ugumu wa kutunza usafi na ukavu wa njia za haja wakati wote. kwa wanaume UTI huongezeka kwa wazee kwasababu ya ongezeko la magonjwa yanayozuia njia ya mkojo.
Magonjwa yanayo zuia njia ya mkojo, mfano
- Mawe kwenye figo au njia ya mkojo kutoka kwenye kibofu kwenda nje (urethra ) .
- Kuongezeka kwa tezi dume na Kuzuia njia ya mkojo kwa wanaume .
- Saratani ya kibofu cha mkojo .
- Kupungua kwa njia ya mkojo kutoka kwenye kibofu kwenda nje (urethra ) kutokana na kovu au kuumia.
- Shida za mishipa ya fahamu inayodhibiti kibofu cha mkojo.
Kukaa na mpira wa mkojo (catheter) kwa mda mrefu bila kubadilishwa na usafi duni wa mpira wa mkojo ni moja ya visababishi vikubwa vya UTI kwa wagonjwa waliolazwa. Kihatarishi hiki huongezeka mara dufu endapo katheta hio itaakaa mfululizo bila kutolewa au kubadilishwa.
Dalili za uti
Dalili za kawaida:
- Maumivu ya kuchoma wakati wa kukojoa (mara nyingi watu husema mkojo unauma)
- Kusikia kubanwa mkojo mara kwa mara lakini mkojo unatoka kidogo tu.
- Mkojo kuwa na harufu kali au kubadilika harufu.
- Maumivu ya sehemu ya chini ya tumbo.
Dalili kali :hizi mara nyingi huashiria maambukizi yamefika kwenye figo.
- Homa (zaidi ya nyuzi joto 38)
- Kichefuchefu na/au kutapika
- Maumivu ya maeneo ya ubavuni (chini ya mbavu) na mgongo.
- Damu kwenye mkojo.
- Usaa kwenye mkojo.
Je UTI ni ugonjwa wa zinaa???
Wakati UTI inaweza kuhusishwa na shughuli za ngono na mara kadhaa kusababishwa na wadudu wanao sababisha magonjwa ya zinaa (kama klamidia na kisonono), UTI siyo ugonjwa wa zinaa moja kwa moja. Magonjwa ya zinaa husambazwa hasa kupitia ngono, wakati UTI inaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na usafi duni au matatizo ya kiafya ambayo hayahusiani na ngono.
Vipimo na matibabu ya UTI.
Wewe au mtu wako wa karibu mkihisi mnazo dalili zilizotajwa hapo juu ni vyema kufika kituo cha afya na kuchukuliwa vipimo ili kuthibitisha ugonjwa na kuanza matibabu.
Vipimo hivyo vinaweza kuwa:
- Kipimo cha mkojo (urinalysis)
- Kuotesha mkojo (urine culture)
- Picha ya damu (full blood picture)
Vipimo vingine vya ziada vinaweza kuongezwa na mtoa huduma ili kuondoa uwezekano wa magonjwa mengine kulingana na dalili au maelezo utakayompa.
Matibabu:
Maambukizi ya mfumo wa mkojo mara nyingi husababishwa na bacteria hivyo matibabu yake hua ni antibiotiki. Mara chache maambukizi hayo husababishwa na fangasi hivyo dawa za fangasi hutolewa kulingana na majibu ya kipimo cha kuotesha mkojo. Dawa zingine zinaweza kuongezwa kulingana na dalili mfano: dawa za maumivu au kushusha homa, dawa za kuzuia kutapika, n.k.
Mbali na matibabu ya hospitali mgonjwa anashauriwa kunywa maji mengi ya kutosha, kula matunda yenye maji maji kama matango na matikiti.
Kurudia kwa UTI.
Maambukizi ya mfumo wa mkojo yanaweza kujirudia mara kwa mara. Hii inaweza kusababishwa na vitu vifuatavyo:
- Maambukizi mapya kutokana na Kurudia tabia hatarishi baada ya ya kumaliza matibabu ( mfano usafi duni)
- Muendelezo wa maambukizi yalele kutokana na kutokumaliza dawa au usugu wa vijidudu kwa dawa.
- Upungufu wa kinga mwilini (mfano kisukari, VVU)
- Kuendelea kuwepo magonjwa mbalimbali kama ya figo au yenye vizuizi kwa njia ya mkojo.
Kumbuka
- Epuka matumizi yakiholela ya antibiotiki !!
- Pata matibabu
- Tumia dawa sahihi
- Maliza dozi yote, tumia dawa kwa usahihi kulingana na maelekezo ya mtoa huduma ili kuzuia kutengeneza usugu wa vijidudu.
Marejeleo:
- Medscape
- NHS UK
- Tanzania standard treatment guideline
- Medical journals
- 1.Medina M, Castillo-Pino E. An introduction to the epidemiology and burden of urinary tract infections. Therapeutic Advances in Urology. 2019;11. doi:10.1177/1756287219832172
- 2. Morris B, Krieger JN. Male circumcision protects against urinary tract infections. Version: 2018-02-16. In: Bjerklund Johansen TE, Wagenlehner FME, Matsumoto T, Cho YH, Krieger JN, Shoskes D, Naber KG, editors. Urogenital Infections and Inflammations. Duesseldorf: German Medical Science GMS Publishing House; 2017-.
- DOI: 10.5680/lhuii000015
Bila shaka umewahi kuusikia ugonjwa uitwao kichocho (bilharzia/schistosomiasis). Je unajua kuwa kichocho ni zaidi ya kukojoa damu tu? Unajua unaambukizwaje na namna gani unaweza kujilinda nao?
Katika makala hii tutajifunza kwa undani kuhusu Kichocho, jinsi kinavyoenezwa, dalili, tiba, madhara ya muda mrefu na jinsi ya kujilinda usiupate.
Kichocho ni nini?
Kichocho ni ugonjwa wa vimelea unaosababishwa na minyoo (trematoda) inayojulikana kama schistosoma.
Kwa makadirio takribani watu milioni 230 duniani kote wameambukizwa na Schistosoma. (Colley, 2014, )
Kichocho ni chanzo kikubwa cha magonjwa na vifo kwa nchi zinazoendelea.
Baada ya malaria, huenda ikawa maambukizi ya vimelea yanayoathiri binadamu kwa uzito zaidi, ikiwa ni endemiki katika takriban nchi 78 na inaathiri takriban watu milioni 240 kila mwaka barani Afrika, Asia, Amerika Kusini, na visiwa vya Karibiani. (Editors of encyclopaedia Britannica ,2024)
Aina za kichocho
Kuna aina kuu mbili za kichocho:
- Kichocho cha utumbo ( intestinal schistosomiasis)
- Kichocho cha mfumo wa mkojo na mfumo wa uzazi ( urogenital schistosomiasis)
Schistosomiasis ya mfumo wa uzazi kwa wanawake ni moja ya magonjwa ya uzazi ambao ni matokeo ya maambukizi ya vimelea vya Schistosoma haematobium na unaathiri angalau wanawake milioni 40, hasa katika Afrika ya Kusini mwa Sahara.(Mazigo HD ,2022)
Maambukizi ya kichocho
Kichocho kwa kawaida huambukizwa kwa kufanya kazi, kuoga, au kuogelea katika maji yenye konokono wanaobeba minyoo ya schistosoma. Minyoo hiyo hupenya kwenye ngozi ya binadamu na kuingia mwilini ambapo hukua kua minyoo wakubwa.Minyoo ya schistosoma hukaa kwenye mishipa ya damu ya binadamu kwa miaka mingi, ikiweza kuiepuka mifumo ya kinga za mwili wakati huo wote minyoo hiyo hutoa mamia hadi maelfu ya mayai kila siku, baadhi ya mayai hutolewa nje ya mwili kupitia kinyesi au mkojo ili kuendeleza mzunguko wa maisha ya vimelea. Mayai mengine yanakwama kwenye sehemu mbalimbali za mwili, na kusababisha mwitikio wa kinga za mwili na kusababisha uharibifu wa viungo vya mwili.
FIG: Mzunguko wa maisha ya minyoo ya schistosoma.
Dalili za kichocho
- Dalili za awali / Acute (katayama fever/syndrome)
Hatua hii husababishwa na mzio (allergic reaction) inayosababishwa na minyoo na/au mayai yao. Dalili hutokea kuanzia wiki 2 hadi 8 baada ya kukutana na maji yaliyoathiriwa.
Dalili zinaweza kujumlisha:
- Maumivu ya tumbo
- kikohozi,
- Homa hasa wakati wa jioni/usiku
- Upele na kuwashwa ngozi (cercarial dermatitis/ swimmer's itch)
- Maumivu ya ini.( sehemu ya tumbo ya juu kulia)
- Damu katika kinyesi na mkojo katika hatua kali zaidi.
2) Dalili za kichocho sugu / chronic
Wagonjwa wenye schistosomiasis sugu huweza kuanza kuonyesha dalili miezi mpaka miaka baada ya kukutana na maji yaliyo athiriwa na minyoo ya schistosoma. Dalili zake hutegemeana na sehemu ya mwili zilizo athirika.
- Dalili za ujumla
- Uchovu wa mwili
- Maumivu ya tumbo
- Kuharisha / kuharisha damu
- Dalili za mfumo wa mkojo
- Maumivu wakati wa kukojoa
- Kukojoa mara kwa mara
- Kukojoa mkojo wenye damu hasa wakati wa kumaliza kukojoa.
- Dalili za Mfumo wa kizazi (kwa wanawake)
- Kutokwa na damu baada ya kujamiana
- Vidonda vya ukeni
- Hedhi isiyo ya kawaida ( irregular)
- Maumivu ya nyonga
- Dalili za moyo na mapafu
- Kikohozi au/na kukohoa damu
- Kubanwa kifua
- Homa
- Kuchoka haraka na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida
- Kupumua kwa shida wakati wa kufanya kazi
- Dalili za ubongo na mishipa ya fahamu
- Maumivu ya kichwa
- kizunguzungu
- Degedege
- kupooza kutokana na mayai kuathiri uti wa mgongo
Vipimo na Tiba
Vipimo vya kichocho vinategemea na dalili na aina ya kichocho, vinaweza kua :
- Kipimo cha mkojo au/na choo kikubwa (kinyesi) ili kuangalia mayai ya minyoo hiyo
- Kipimo cha damu ( full blood picture)
- Ultrasound ( tumbo, pelvic)
- X-ray ( tumbo, kifua)
- Uchunguzi wa kibofu cha mkojo kwa kutumia cystoscope
- CT scan , MRI kwa ajili ya kugundua maambukizi ya ubongo na uti wa mgongo
Matibabu makuu ya kichocho ni dawa ya kuua vimelea mwili ambayo ni dozi ya mara moja, lakini unaweza kupewa dawa zingine kuligana na dalili zako.
Mfano: dawa za allergy, dawa za kushusha homa, dawa za kuzuia degedege n.k
Madhara ya kichocho
- Kifafa au degedege
- Tumbo kujaa maji(ascites) na kutapika damu ( husababishwa na portal hypertension)
- Saratani ya Kibofu cha mkojo
- Kuvuja damu katika mfumo wa chakula ( gastrointestinal bleeding)
- Ugonjwa wa mapafu na moyo unaoweza kupelekea moyo kushindwa kufanya kazi vizuri
- Kupooza
- Schistosomiasis sugu ya mfumo wa uzazi imehusishwa na ugumba, ujauzito wa nje ya mfuko wa uzazi ( ectopic), kuharibika kwa mimba, kujifungua kabla ya wakati, na uzito mdogo wa watoto wachanga.(Mazigo HD ,2022)
- Zaidi ya hayo, ushahidi unaoongezeka unaonyesha kwamba Schistosomiasis ya mfumo wa uzazi kwa Wanawake huongeza hatari ya kupata virusi vya ukimwi (HIV) na HPV/Saratani ya shingo ya kizazi.(Mazigo HD ,2022)
Hitimisho
Tunaweza kuepuka kuugua kichocho kwa
- kuepuka kuogelea au kuoga katika mabwawa, mito, maziwa na madimbwi.
- Lakini pia watu wote wanaofanya kazi katika vyanzo vya maji baridi au maji yaliyo tuama ( wavuvi, wakulima wa mpunga nk) watumie nyenzo za kujikinga kama gloves na boots.
- Watu wanaotumia maji ya mto / ziwa kufanyia shughuli mbalimbali (kama kufua, usafi wa majumbani,kuoga,) watibu maji hayo kabla ya kutumia ( kuchemsha au kwa dawa)
Pata matibabu mapema unapokuwa na dalili za kichocho na tumia dawa kama utakavyoelekezwa na mtoa huduma wa afya ili kuepuka kichocho sugu na madhara yanayotokana na kichocho.
Marejeleo
- Medscape
- Human schistosomiasis
Colley, Daniel G et al.
The Lancet, Volume 383, Issue 9936, 2253 - 2264 - Britannica, T. Editors of Encyclopaedia (2024, August 6). schistosomiasis. Encyclopedia Britannica. https://www.britannica.com/science/schistosomiasis
- Mazigo HD, Samson A, Lambert VJ, Kosia AL, Ngoma DD, Murphy R, et al. (2022) “Female genital schistosomiasis is a sexually transmitted disease”: Gaps in healthcare workers’ knowledge about female genital schistosomiasis in Tanzania. PLOS Glob Public Health 2(3): e0000059. https://doi.org/10.1371/journal.pgph.0000059
Makala hii iliandikwa na Dada Subi wa tovuti ya wavuti.com akizungumzia kuhusu umuhimu wa kufanyika kwa utafiti juu ya dhana ya kuwepo kwa uwezo wa mafuta ya nazi katika kutibu na kuzuia ugonjwa wa kusahau wa Alzheimer's unaowaathiri zaidi wazee. Ungana naye katika maoni yake haya.
Baadhi ya watafiti wanasema kiwango fulani cha mafuta ya nazi ni muhimu kwenye chakula kwa kuwa husaidia kupunguza ugonjwa wa kusahau "Alzheimer's" ambao mara nyingi humjia mwanadamu kadiri umri unavyosogelea uzeeni.
Watafiti wanathubutu kusema, huenda mafuta haya ya nazi yakazuia kabisa kupata ugonjwa huo kwa baadhi ya watu.
Ingekuwa vyema na sisi Tanzania tukafanya utafiti kwa jamii ya watu wanaotumia kwa wingi mafuta ya nazi katika mapishi yao, hasa wale waishio mikoa ya mwambao wa pwani ambapo zao ma mnazi hustawi vizuri na kwa wingi.
Pengine hii ikawa pia sababu kujibu suala la kwa nini yapo matukio mengi ya Wazee na Vikongwe wengi kuuawa kikatili katika mikoa kadhaa nchini Tanzania ambayo zao la nazi ni nadra kuonekana sokoni, achilia mbali kutumika kama kiungo katika mapishi na/au matumizi ya kuchua na marashi.
Nimewaza hivyo kwa kuwa wazee wetu wanaouawa mara nyingi utetezi unaotolewa na wauaji ni kuwa mzee alikuwa na "dalili" za uchawi kwa kuwa pengine alikuwa akisema mwenyewe kama mwehu, akiondoka usiku na kutokomea pasikojulikana, alikuwa akivua nguo mbele ya kadamnasi, alikuwa mwoga au kuonekana mwenye wasiwasi wakati wote n.k., bila watu hao kufahamu kuwa kwa ujinga* wa masuala ya afya ya akili ya binadamu yatokanayo na umri, matukio mbalimbali maishani yaliyoathiri akili na fikira, pamoja na hofu ya uzee kwa vitendo walivyotendewa wengine, wanaweza kabisa kuwa sababu ya matatizo (dalili) na kuishia kuwawahukumu baadhi ya wazee hao kifo pasina hukumu ya haki. Ninaamini kuwa, kama ambavyo wapo waliofungwa jela kwa makosa ya kudhaniwa, kusingiziwa, wasiyoyatenda na visasi, vile vile wapo wanaouawa kwa sababu zizo hizo.
Niseme kuwa, zinazotajwa kuwa sababu (naita visingizio) za kumtuhumu mtu uchawi zinalandana na dalili za ugonjwa wa kusahau "Alzheimer's disease" ambazo niliwahi kuziandika wakati nikichangia makala za afya katika gazeti la KwanzaJamii (unaweza kuzisoma kwa lugha ya Kiingereza katika linki hii: alz.org).
Makala hii ni kwa hisani ya wavuti.com
Polio ni ugonjwa wa kuambukiza usababishwao na virusi, huathiri neva na kusababisha ulemavu.
Kutokana na taarifa za shirika la afya duniani:
- Polio huathiri zaidi watoto wa umri wa chini ya miaka mitano
- Ulemavu hutokea kwa mmoja kati ya maambukizi 200
- Mpaka 2013 ni nchi tatu ambazo bado kuna mlipuko wa ugonjwa huu wa kupooza Afghanistan, Pakistan na Nigeria. Ila kutokana na Taarifa kutoka wizara ya afya ya Tanzania ilipokea taarifa kutoka shirika la afya duniani kuwa kuna mlipuko katika nji jirani ya Kenya, wilaya ya Fafi.
Je ni zipi dalili za ugonjwa huu?
Dalili hizi hudumu kwa kati ya siku 1 hadi 10
- Homa
- Maumivu ya kichwa
- Kutapika
- Uchovu
- Maumivu ya shingo
- Maumivu ya mgongo
- Maumivu ya mikono na miguu
- Misuli kukakamaa
Je ni matatizo gani mtu huweza kupata baada ya maambukizi haya?
- Kupooza misuli
- Ulemavu wa miguu
Kati ya maambukizi yanayowasumbua wanawake wengi duniani ni maambukizi ya fangasi. Inakisiwa asilimia 75 ya wanawake wote duniani hupata maambukizi haya katika kipindi cha uhai wao.
Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na uwepo wa fangasi wanaojulikana kitaalamu kama Candida albicans. Maambukizi haya pia hujulikana kama yeast infection au thrush. Fangasi hupatikana kama vimelea vya kawaida katika mdomo, mpira wa kupitisha chakula sehemu inayojulikana kama pharynx, katika kibofu cha mkojo, uume na hata kwenye uke.
Mfumo mzuri wa kinga wa mwili pamoja aina fulani za bakteria wanaoishi pamoja na fangasi hawa husaidia sana katika kuthibiti maambukizi yanayoyosababishwa na aina hi ya fangasi.
Nini hutokea?
Kwa kawaida, Candida albicans huishi kwenye uke na sehemu nyingine (kama zilivyoelezewa hapo juu) bila kusababisha madhara yoyote yale isipokuwa pale mazingira ya eneo husika yanapobadilika kama vile mabadiliko katika hali ya pH ya eneo husika (ifahamike ya kwamba pH ya kawaida ndani ya uke ni 4.0 - 4.5) au uwiano wake na vimelea (microorganisms) wengine unapoharibiwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya madawa aina ya antibiotics, kupungua kwa kinga mwilini kutokana na magonjwa mbalimbali n.k.
Maambukizi haya ya fangasi yanaweza kugawanywa katika sehemu kuu mbili
- Maambukizi yasiyo makali yaani uncomplicated thrush: Katika kundi hili, mgonjwa hupatwa na maambukizi mara moja hadi nne kwa mwaka na dalili zake huwa si mbaya sana na maambukizi haya husababishwa na fangasi wa jamii hii ya Candida albicans.
- Maambukizi makali yaani complicated thrush: Katika kundi hili, mgonjwa hupatwa na maambukizi zaidi ya mara nne kwa mwaka, dalili zake kuwa mbaya zaidi au kama maambukizi yatakuwa yametokea kipindi cha ujauzito, ugonjwa wa kisukari, upungufu wa kinga mwilini. Aina hii kusababishwa na vimelea vya aina nyingine tofauti na Candida albicans.
Vihatarishi
Watu walio katika hatari ya kupata maambukizi ya fangasi hawa ni wale wenye
Mchungaji Mstaafu Ambilikile Mwasapile ni jina lililojipatia umaarufu sana katika miezi ya hivi karibuni nchini Tanzania na eneo la nchi za maziwa makuu. Umaarufu wake unatokana na madai kuhusu uwezo wake wa kutibu maradhi sugu mbalimbali kwa kutumia dawa ya ‘kiimani’ iliyotengenezwa kwa kutumia majani ya mti maarufu sana katika mazingira ya eneo hilo unaojulikana kama mugariga.
Lakini mugariga ni nini? Tabia zake ni zipi? Je una uwezo wowote wa kutibu maradhi yanayodaiwa kuwa sugu? Ni mti wa kale au umegunduliwa juzi juzi tu?
Mugariga au Carissa edulis kama unavyojulikana kitaalamu au ‘mtanda-mboo’ kwa Kiswahili fasaha si kitu kigeni duniani. Ni mti ambao umekuwepo tangu zama na zama. Kiasili, mti huu unapatikana maeneo mengi sana duniani hasa yale yenye uoto wa kitropiki kama vile Kenya, Tanzania, Sudan, Ethiopia, Thailand, Botswana, Namibia, Myanmar na Afrika ya Kusini (1).
Mti huu upo kwenye familia ya mimea ya Apocynaceae, familia ambayo inajumuisha genera zipatazo 163 za mimea zenye takribani aina 1850 za miti (2). Familia ya Apocynaceae inajumuisha aina kadhaa za miti ambazo zina matumizi mbalimbali kulingana na sehemu zinapopatikana. Kwa mfano kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 1970 na Kokwaro na wenzake huko nchini Kenya (3), ilionekana kuwa aina ijulikanayo kama Acokanthera schimperi imekuwa ikitumiwa kwa miaka mingi na wenyeji wa maeneo ulipofanyika utafiti huo kama sumu kwa kupaka kwenye ncha za mishale na mikuki kwa ajili ya kutumika kama silaha. Hata hivyo, zipo aina kadhaa katika familia hii ya mimea ambazo si sumu na zimekuwa zikitumiwa kwa matumizi mbalimbali yakiwemo chakula.
Matumizi ya mti wa Carissa edulis yanatofautiana kati ya jamii na jamii. Kwa mfano inasemekana baadhi ya jamii nchini Ghana hutumia mti huu kama chachandu ya kuongeza ladha katika chakula, wakati nchini Sudan na Kenya, mti huu hutumika kutengenezea siki au jam. Aidha zipo jamii kadhaa hukohuko Kenya zinazotumia mti huu kama dawa ya kufukuza nyoka kwa kuweka mizizi yake iliyokaushwa juu ya paa la nyumba.
Pamoja na matumizi yaliyoelezwa hapo juu, matumizi makubwa kabisa ya mti ambayo ndiyo msingi mkuu wa makala hii ni katika kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu pamoja na wanyama.
Ili tuweze kufahamu vizuri utendaji wake kazi katika matibabu, hebu kwanza tuangalie kilichomo (ingredients) katika mti huu.
Kemikali zilizomo kwenye mti huu (ingredients)
Vifuatavyo ni viasili vilivyowahi kukutwa katika mti wa Carissa edulis baada ya tafiti mbalimbali za wataalamu wa afya pamoja na mitishamba.
- Mizizi yake imegundulika kuwa na kiasili cha Sesquiterpene ambacho huzalisha viasili vya carissone, cryptomeridiol, germacarane na β-eudesmane. Kwa ujumla viasili vya sesquiterpenes vinajulikana kuwa na tabia au uwezo wa kutibu magonjwa au hali zote zinazohusiana na mcharuko mwili (anti-inflammatory effects), vimelea (antimicrobial effects) na saratani na uvimbe (antineoplastic effects).
- Mbegu za matunda yake zimeonekana kuwa na viasili vya lignans kama vile carissanol, secoisolariciresinol, nortrachelogenin na olivil. Kutokana na umbo lake la kikemikali, viasili hivi hususani carissanol vimeonekana kuwa na tabia au uwezo wa kuua vimelea (antimicrobial effects) na kusaidia kuua seli zisizohitajika mwilini (antioxidant effects) sifa ambayo inaipa uwezo mkubwa wa kupambana na seli za saratani.
- Vichipukizi vyake vina viasili vya quebrachytol ambavyo kina tabia za kuimarisha kinga ya mwili kwa kutegemeza tando za seli (membrane stabilization effects) na kuua seli zisizohitajika zikiwemo za saratani (antioxidant effects). Pia zina cardioglycosides ambavyo hufanya kazi kwenye pump ya Na+-K+ na kuweza kuua minyoo.
- Shina na majani yameonekana kuwa na aina fulani ya kemikali ya alkaloid
- Magamba ya mizizi yake yamegunduliwa kuwa na viasili vya 2-Hydroxy acetophenone ambacho kina uwezo wa kufanya kazi katika mishipa ya damu na kuifanya itanuke (vasodilation effects) na hivyo kuwa na sifa kubwa ya kusaidia kushusha shinikizo la damu na kuongeza nguvu za kiume.
Matumizi katika tiba
Wenyeji wa jamii kadhaa nchini Ghana wamekuwa, kwa miaka kadhaa sasa, wakichanganya magamba ya mizizi na baadhi ya viungo na kutumia kwa ajili ya kutibu maumivu ya mgongo na maumivu ya sehemu nyingine za mwili. Aidha nchini Guinea, jamii zimekuwa na mazoea ya kuchemsha majani ya mti huu na kutumia kutibu maumivu ya meno. Jamii nyingine barani Africa zimekuwa zikitumia sehemu ya juu ya mizizi hii kutibu uvimbe na mcharuko mwili (inflammatory reactions). Hali kadhalika sehemu za mizizi mkuu zimekuwa zikitumika kwa ajili ya kutibu magonjwa ya zinaa kama kaswende na kisonono, kurudisha urijali na kuongeza uwezo wa kuzaa, vidonda vya tumbo au kikohozi.
Jamii nyingine zimekuwa zikitumia mti huu kwa ajili ya kutoa mimba, na kwa hapa Tanzania yapo baadhi ya makabila yanayotumia Carissa edulis kutibu ugonjwa wa malaria.
Utafiti wa hivi karibuni nchini Kenya umeonesha kuwa, mti wa Carissa edulis una uwezo wa kuua vimelea vya virus aina ya Herpes Simplex Virus ingawa haijajulikana hasa ni kwa njia gani.
Kwa mujibu wa mtafiti Lindsay na wenzake, 2000 (3) ukiacha aina (species) hii ya Carissa edulis, aina nyingine zilizo katika jamii moja na mti huu, kama vile Carissa lanceolata, imethibitika kuwa na uwezo wa kutibu bacteria vya aina mbalimbali vikiwemo Staphylococcus aureus, Escherichia coli na Pseudomonas aeruginosa bila kuwa na madhara kwa mtumiaji.
Je mti huu una madhara kwa afya za binadamu?
Mpaka sasa hakuna ushahidi wowote wa kitafiti unaoonesha kuwa matumizi ya dawa za mitishamba zinazotokana na mti wa Carissa edulis zina madhara kwa binadamu.
Je kuna ushahidi wowote wa kitafiti kuthibitisha uwezo wa Carissa edulis?
Tafiti kadhaa zilizofanywa barani Afrika na kwingineko duniani zinathibitisha hilo.
1. Uwezo wa kupambana na virus (Antiviral activities)
Mwaka 2005 , watafiti nchini Kenya (4) walitumia magamba ya mizizi ya Carissa edulis kuchunguza uwezo wa mti huu katika kupambana na virus wa jamii ya Herpes Simplex Virus (HSV) kwa kutumia panya. Matokeo ya utafiti huo yalionesha kuwa, dawa iliyotumika kutokana na mti huo ilikuwa na uwezo wa kuua aina (strains) zote mbili (wild na resistant) za virus hawa wa HSV. Ilionekana pia kuwa, aina sugu ya virus hawa yaani resistant strain ndiyo iliyoathiriwa zaidi ikilinganishwa na aina isiyo sugu (wild strain). Kwa maneno mengine, mti huu ulionekana kuwa na uwezo mkubwa katika kuua na kutokomeza virus walioonekana kuwa sugu zaidi kwa madawa mengine kuliko wale wasio sugu. Hata hivyo watafiti hawakuonesha ni kwa jinsi gani (mode of mechanism) mti huu uliweza kufanya kazi hiyo na hivyo kupendekeza kufanyika kwa utafiti mwingine utakaofanya kazi hiyo hususani kwa binadamu.
2. Uwezo wa kupambana na virus vya Ukimwi (Antiretroviral effects)
Mpaka sasa hakuna utafiti wowote wa kisayansi uliofanywa kuthibitisha uwezo wa mti wa Carissa edulis katika kupambana na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi. Hivyo bado ni ngumu kuthibitisha uwezo wa mti huu katika kuua na kutokomeza virus vya Ukimwi. Hii inaleta changamoto kubwa kwa wanasayansi kuweza kubainisha hilo.
3. Uwezo wa kutibu kifafa na degedege (Anticonvulsant effects)
Mtafiti Ya’u (5) kutoka idara ya madawa ya chuo kikuu cha Ahmadu Bello, nchini Nigeria akishirikiana na wenzake walifanya utafiti kuchunguza uwezo wa mti wa Carissa eduliskatika kutibu magonjwa ya degedege na kifafa. Katika utafiti wao, walitumia magamba ya mizizi ya mti huu kuchunguza uwezo wake katika kuzuia kutokea kwa degedege kwa wanyama. Watafiti hao walipendekeza kuwa mti wa Carissa edulis una kiasili chenye uwezo wa kuzuia kutokea kwa degedege na hivyo kukubaliana na madai ya baadhi ya jamii zinazotumia mti huu kama dawa ya kutibu tatizo hilo.
4. Uwezo wa kutoa na kupunguza maji mwilini (Antidiuretic effects)
Mtafiti Nadi T (6) wa chuo kikuu cha Addis Ababa, Ethiopia akishirikiana na wenzake walifanya utafiti kuchunguza uwezo wa mti Carissa edulis katika kutoa na kupunguza maji mwilini kwa njia ya mkojo (antidiuretic effects). Katika utafiti wao, wataalamu hao walitumia magamba ya mizizi kuwapa panya na kisha kuchunguza kiasi cha mkojo kilichotolewa na panya hao pamoja na upotevu wa viasili vya Sodium, potassium na Chloride mwilini. Kadiri dozi ya dawa iliyotumika ilipoongezwa, kiwango cha mkojo na upotevu wa viasili hivyo nao pia uliongezeka. Matokeo haya ya utafiti yanaendana na mazoea ya tangu kale ya jamii mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia mti huu kwa ajili ya kusaidia kukojoa hususani kwa watu wenye matatizo ya figo.
5. Uwezo wa kutibu kisukari (Antidiabetic effects)
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Alexandria nchini Misri (7), wakitumia panya wa maabara, walifanya utafiti kwa lengo la kuchunguza uwezo wa mti wa Carissa eduliskatika kutibu ugonjwa wa kisukari. Katika utafiti wao, wataalamu hao walifanikiwa kugundua kuwa, majani ya mti wa Carissa edulis yalikuwa na uwezo wa kushusha na kurekebisha kiwango cha sukari kwa panya waliokuwa na kisukari ndani ya muda wa masaa matatu, sawa kabisa na dawa za Metformin na buguanides zinazotumika kutibu ugonjwa huo mahospitalini.
Hitimisho
Ingawa tafiti mbalimbali za kisayansi zimefanyika kujaribu kuonesha uwezo wa mti waCarissa edulis katika kutibu magonjwa kadhaa kwa kutumia wanyama kama panya na kuku, mpaka sasa hakuna utafiti wowote uliowahi kufanyika kwa binadamu kuthibitish hilo, pamoja na kwamba tangu enzi na enzi, watu wa jamii zilizojaliwa kuwa na mti huu wamekuwa na wanaendelea kuutumia katika kujitibu maradhi mbalimbali yanayowakabili. Ni changamoto kwa watafiti na watalaamu kufanya tafiti zaidi za kisayansi ili kutambua jinsi mti huu unavyofanya kazi katika kutibu baadhi ya magonjwa na kuthibitisha pasi shaka uwezo wake katika kutibu ugonjwa wa Ukimwi na maradhi mengine sugu.
Marejeo
- www.worldagroforestry.org/treedb2/AFTPDFS/Carissa_edulis.pdf
- Leeuwenberg, A.J.M. & Kupicha, F.K. et al. (1985) Apocynaceae FZ 7(2)
- Kokwaro, J.O., 1976. Medicinal Plants of East Africa. East African Literature. Bureau, Nairobi, Kenya, pp. 1–8, 25–26.
- Lindsay, E.A., Berry, Y., Jamie, J.F., Bremner, J.B., 2000. Antibacterial compounds fromCarissa lanceolata R. Br. Phytochemistry 55, 403–406.
- Festus M. Tolo, Geoffrey M. Rukunga, Faith W. Muli, Eliud N.M. Njagi, Wilson Njue, Kazuko Kumon, Geoffrey M. Mungai, Charles N. Muthaura, Joseph M. Muli, Lucia K. Keter, Esau Oishi, Mawuli W. Kofi-Tsekpo, 2005. Anti-viral activity of the extracts of a Kenyan medicinal plant Carissa edulis against herpes simplex virus. Journal of Ethnopharmacology 104 (2006) 92–99. Inapatikana mtandaoni www.sciencedirect.co
- Ya’u J, Yaro AH, Abubakar MS, Anuka JA, Hussaini IM., 2008. Anticonvulsant activity of Carissa edulis (Vahl) (Apocynaceae) root bark extract. J Ethnopharmacol. 2008 Nov 20;120(2):255-8. Epub 2008 Sep 4. Inapatikana mtandaoni www.sciencedirect.com
- Nedi T, Mekonnen N, Urga K., 2004. Diuretic effect of the crude extracts of Carissa edulis in rats. J Ethnopharmacol. 2004 Nov;95(1):57-61. Inapatikana mtandaoni www.sciencedirect.com
- El-Fiky FK, Abou-Karam MA, Afify EA., 1996. Effect of Luffa aegyptiaca (seeds) and Carissa edulis (leaves) extracts on blood glucose level of normal and streptozotocin diabetic rats. J Ethnopharmacol. 1996 Jan;50(1):43-7. Inapatikana mtandaoni http://www.kau.edu.sa
Ni tatizo la ngozi ambalo linaifanya ngozi kuwa nyekundu, kuvimba/kuwasha au kupata mcharuko (inflammation) baada ya kugusana na kitu kinachochangia mwili kucharuka au kupata mzio (allergic reaction)
Kuna msomaji mmoja aliuliza swali kwenye tovuti hii, na hapa na nukuu swali lake ‘’ Nina tatizo la kutoka vipele sehemu za siri siku moja baada ya kufanya mapenzi au baada ya "masterbartion". Vipele hukaa siku tatu hadi nne hutumbuka na kutoa maji, kidonda hukauka siku moja hadi mbili bila dawa. Nimepima ukimwi pamoja na kaswende lakini halikuonekana tatizo. Naomba msaada kujua tatizo langu’’ Mwisho wa kunukuu.
Muundo ya moyo na mishipa ya damu ni mojawapo ya vinavyooathirika katika magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo. Vijusi(fetuses) kati ya 8 hadi 10 huathirika kwa kila 1000.
Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo huweza kutoa dalili mara tu baada ya kuzaliwa, utotoni na wakati mwingine husubiri mpaka ukubwani.
Magonjwa ya Moyo ya Kuzaliwa husababishwa na nini?
Kwa wengi sababu huwa haijulikani. Ila huwa kuna vitu hatarishi ambavyo hupelekea kuongezeka kwa uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo, vitu hivyo hatarishi ni:
- Matatizo ya kijenetekia utotoni kama Downs syndrome, Turner’s syndrome, Marfan syndrome,
- Matumizi ya dawa ya kutibu chunusi (acne) aina ya retinoic acid, madawa ya kulevya na unywaji wa pombe wakati wa ujauzito
- Maambukizi ya virusi vya Rubella (German measles) kipindi cha kwanza cha ujauzito (1st trimester)
Kuna aina mbili za magonjwa ya moyo ya kuzaliwa
- Cyanotic
- Non-cyanotic
Cyanosis ni hali ya kuwa na rangi ya samawati (katika midomo,ulimi, ganja za mikono na miguuni) kutokana na kukosa oksijeni ya kutosha mwilini.
Cyanotic
Magonjwa ya moyo ya asili ambayo yanaangukia katika kundi hili ni pamoja na
- Tetralogy of fallots
- Transposition of great vessels
- Tricuspid atresia
- Total anomalous pulmonary venous return
- Truncus arteriousus
- Hypoplastic left heart
- Pulmonary atresia
- Ebstein anomaly
Non-cyanotic
Magonjwa ya moyo ya asili yaliyo kwenye kundi hili hujumuisha
- Ventricular septal defect (tundu katika kuta za ventrikali)
- Atrial septal defect (tundu katika kuta za atria)
- Patents ductus arteriousus
- Aortic stenosis
- Pulmonic stenosis
- Coarctation of the aorta
- Atrioventricular canal (endocardial cushion defect)
Dalili za Magonjwa ya Moyo ya Kuzaliwa
Kwa ujumla, wagonjwa wa moyo wa asili huwa na dalili zifuatazo
- Kupumua kwa shida
- Kushindwa kula vizuri
- Matatizo ya ukuaji
- Matatizo ya ukuaji wa misuli ya mikono na miguu
- Maambukizi ya mfumo wa hewa
- Cyanosis kwa aina ya kwanza(rangi ya samawati katika midomo,ulimi, viganja vya mikono na miguuni)
- Ongezeko la sauti ya ziada katika sauti za moyo kutokana na tatizo (heart murmur)
- Mabadiliko kwenye kucha hasa za vidole vya mikononi (digital clubbing)
Vipimo na Uchunguzi
Baadhi ya vipimo vinavyotumika kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa haya ni
- Echocardiogram/transesophageal echocardiogram
- Cardiac catheterization
- Magnetic Resonance Imaging
- Electrocardiogram
- Chest x-ray
Matibabu
Matibabu hutegemea aina ya ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa nao, hivyo hapa nitaelezea kwa kifupi ila, maelezo zaidi nitatoa katika makala zinazokuja za ugonjwa mmoja mmoja.
Aina nyingi za magonjwa haya huwa na madhara makubwa hivyo huhitaji upasuaji kurekebisha kasoro hizo, pamoja na matibabu ya dawa (diuretics ambazo husaidia kupunguza maji na chumvi mwilini, digoxin ambayo husaidia kuongeza nguvu katika mapigo ya moyo).
Vilevile kuna tiba nyengine ambayo badala ya upasuaji kitaalamu Transcatheter ambapo kifaa cha kufunga au kupachika huwekwa kwenye catheter maalumu ambayo hupita kwenye mishipa ya damu mpaka kwenye kasoro na kurekebisha kwa kuziba tundu nakadhalika.
Kuna aina mbili kuu za hiatus hernia
- Sliding type : Kama jina lake linavyomaanisha, aina hii hutokea iwapo sehemu ya juu ya utumbo inaposukumwa juu na kuingia kwenye upenyo wa esophagus hiatus baada ya kutokea kwa ongezeko la presha katika maeneo ya tumbo (increased pressure in the abdominal cavity) na kurudi kama kawaida wakati presha inapopungua.
- Fixing type: Aina hii hutokea iwapo sehemu ya juu ya utumbo inapokuwa kwenye maeneo ya kifua na haishuki chini.
Vihatarishi vya Ugonjwa huu
- Kunyanyua vitu vizito au kuinama sana
- Kukohoa sana au kukohoa mara kwa mara kutokana na sababu mbalimbali
- Kutapika sana (violent vomiting)
- Kupiga chafya sana (Hard sneezing)
- Ujauzito -Kutokana na mfuko wa uzazi (uterus) kusukuma viungo kwenda juu kutokana na kuongezeka ukubwa wake.
- Wakati wa kujifungua- Kutokana na kuongezeka kwa presha ndani ya tumbo wakati mama anajitahidi kusukuma mtoto. Si wanawake wote wanaopata tatizo hili.
- Kujikamua wakati wa kwenda haja kubwa (straining during constipation)
- Uzito uliopitiliza -Kutokana na kuongezeka uzito ambao unasukuma viungo kwenye maeneo ya kifua kwenda chini na hivyo kuongeza presha tumboni.
- Kujisaidia haja kubwa wakati mtu amekaa - Kutokana na maendeleo ya binadamu, watu wengi sasa hivi wameanza utamaduni wa kutumia vyoo vya kukaa wakati wa kujisaidia haja kubwa, katika tafiti iliyofanywa na Dr Denis Burkitt (1), imeonekana ya kwamba kujisaidia wakati mtu amekaa hufanya mtu kujikamua zaidi na hivyo kuongeza presha ndani ya utumbo (Increased intraabdominal pressure) na hivyo kusukuma mfuko wa kuhifadhia chakula (utumbo) kupitia kwenye upenyo wa esophagus hiatus na hivyo kusababisha hiatus hernia.
Tatizo la kurithi (Heredity)
- Uvutaji sigara
- Matumizi ya madawa ya kulevya kama cocaine
- Kuwa na kiwambo hewa (diaghram) dhaifu
- Msongo wa mawazo (depression)
- Matatizo ya kuzaliwa (congenital defects).
Dalili na Viashiria
- Maumivu ya kifua
- Kichomi (pleurisy) ambacho kinakuwa kikali sana wakati wa kuinama au mtu anapolala chini
- Matatizo katika kumeza chakula
- Kupumua kwa shida Kutokana na hiatus hernia kupunguza uwezo wa ufanyaji kazi wa kiwambo hewa (diaphragm).
- Mapigo ya moyo kwenda kasi Kutokana na mkwaruzo wa neva inayojulikana kama vagus nerve.
Mara nyingi sana hiatus hernia haioneshi dalili zozote zile isipokuwa inapokuwa kubwa sana. Maumivu na kichomi hutokana na kurudishwa kwa tindikali ya kwenye tumbo (gastric acid) kwenye kifua. Pia tindikali aina ya bile acid na hewa huwa inasukumwa juu kwenye kifua.
Vipimo vya Uchunguzi
- Barium Swallow X-ray – X-ray ya kuangalia viungo vya ndani, mgonjwa hupewa au huchomwa sindano yenye dawa maalum ambayo huonekana vizuri kwenye X-ray, na baada ya hapo hupigwa picha za X-ray akiwa amekaa au amesimama. Kawaida kipimo hiki huchukua masaa 3-6.
- Esophagogastroduodenoscopy (OGD) - Mpira maalum wenye taa na camera kwa mbele unaoingizwa mdomoni kwenye mpira wa kupitisha chakula (esophagus) na hutazama kama kuna magonjwa yoyote kwenye esophagus hadi kwenye sehemu inayojulikana kama duodenum.
- Electrocardiography (ECG)- Kipimo cha kuangalia kama kuna matatizo katika jinsi moyo unavyopiga
- Chest X-ray- Kuangalia kama kuna magonjwa kama homa ya mapafu (Pneumonia), kama kuna pafu lolote ambalo halifanyi kazi, madhara kwenye moyo (injury to the heart) na pia kuangalia matatizo yoyote yale.
- Complete Blood Count- Kipimo cha kuangalia wingi wa damu, kuangalia aina mbalimbali za chembechembe za damu kama zipo katika maumbo yao ya kawaida, wingi wao kama ni wa kawaida.
Tiba ya Hiatus Hernia
- Dawa za kuyeyusha tindikali mwilini (antacids) hutumika kama Gelusil, Maalox nk.
- H2 receptor antagonist –Dawa zinazopunguza kiwango cha utolewaji wa tindikali kama cimetidine, ranitidine nk.
- Dawa ambazo huzuia utolewaji wa tindikali na kuponya tishu za esophagus (Proton Pump Inhibitors) dawa hizi ni omeprazole, lansoprazole nk.
Madhara ya Hiatus Hernia
- Kichomi
- Ugonjwa wa esophagitis
- Barretts esophagus
- Saratani ya kwenye mpira wa kupitisha chakula (esophageal cancer)
- Kuoza kwa meno (dental erosion)
- Strangulation of the stomach (kunyongwa kwa sehemu ya juu ya tumbo na hivyo kusababisha sehemu hii kukosa damu ya kutosha na hivyo tishu zake kufa na kuoza (ischemic and necrosis)
- Kuzuia pafu kujaa hewa na hivyo kushindwa kutanuka na kusababisha mtu kupumua kwa shida sana.
Jinsi ya kujikinga
- Kuacha kunywa pombe
- Kuacha matumizi ya madawa ya kulevya kama cocaine
- Kupunguza uzito uliopitiliza.
- Kula milo midogo mara nyingi kwa siku
- Epuka vyakula vinavyoongeza kichomi kama chocolate, vitunguu, vyakula vikali, vinywaji venye limau, ndimu nk.
- Kula chakula cha usiku masaa matatu kabla ya kwenda kulala
- Pumzika kwa kukaa baada ya kula usilale chini.
- Nyanyua sehemu unayoweka kichwa chako wakati wa kulala kwa angalau 15cm (6 inches)
- Punguza msongo wa mawazo
- Acha kuvuta sigara.
Marejeo
Hatari ya Kukakamaa kwa mwili huongezeka kwa mtu mwenye kiharusi au vihatarishi vya kiharusi kutokana na utafiti uliofanywa Rotterdam uholanzi.
Sehemu ya ubongo kitaalamu Cerebral cortex inapokandamizwa aidha na kihararusi cha mishipa kuchanika na kuvujisha damu au mishipa inapoziba husababisha Kukakamaa kwa mwili. Hali yoyote isababishayo upungufu wa damu kufika katika sehemu za ubongo hupelekea Kukakamaa kwa mwili kutokea, na moja wapo ya sababu hizo ni magonjwa ya moyo.