Takwimu zilionyesha kuongezeka kwa kiwango cha kuzaliwa kwa watoto waliokuwa na uzito mdogo chini ya gramu 1000. Wamama wote waliokuwa na afya nzuri ya kinywa na meno walijifungua watoto wenye uzito wa zaidi ya gramu 1000.Asilimia sita (6) ya wamama wenye afya dhaifu ya kinywa na meno walijifungua watoto wenye uzito wa chini ya gramu 1000 huku asilimia 11.4 ya wamama wenye afya mbaya ama afya mbaya zaidi ya kinywa na meno walijifungua watoto wenye uzito mdogo zaidi wa chini ya gramu 1000. Tafiti zilizofanyika kwenye mataifa ya Poland, Ufaransa na Brazil yalionyesha matokeo yanayokaribiana na haya.
Matokeo ya utafiti huu yanaahusika na kuharibika kwa ujauzito ndani ya miezi sita ya awali ya mimba, kuharibika kwa mimba katika hatua za mwishoni na hata kujifungua mtoto njiti. Tatizo la magonjwa ya fizi kusababisha kuharibika kwa ujauzito na kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo wa chini ya gramu 1000 linatokea kwa zaidi ya njia moja,kimsingi magonjwa ya kinywa na meno yanaruhusu bakteria waliomo kinywani kujipenyeza kwenye fizi na kuingia kwenye mfumo wa mzunguko wa damu, bakteria hawa wa kinywani wanapoingia kwenye mfumo wa damu husababisha kuganda kwa damu iliyopo kwenye mzunguko na hivyo kusababisha kiharusi/stroke. Bakteria hawa pia husababisha maambukizi kwenye kuta nyembamba za ndani ya moyo pamoja na valvu za moyo na moyo. Ugonjwa wa fizi usipotibiwa mapema unakomaa zaidi na kushambulia chembehai zinazoshikilia jino kwenye taya. Mara nyingine taya huathirika pia, ugonjwa hii ni hatari sana kwa ukuaji wa mimba.
Habari njema ni kuwa, ikiwa ugonjwa wa fizi utagunduliwa na kudhibitiwa mapema, hatari zote za kuharibika ujauzito ama kujifungua mtoto njiti unatoweka,
Utafiti uliofanyika Chile kuchunguza afya ya kinywa na meno miongoni mwa wamama watarajiwa wapatao 400, wenye umri kati ya miaka 18 na 35 kwa umri wa majuma ya ujauzito yasiyozidi 28. Madaktari wa meno waliwatibu wamama watarajiwa wapatao 200 mara tu baada ya uchunguzi, vile vile walitibu wamama wengine 200 mara tu baada ya kujifungua.
Matokeo yalionyesha kuwa kiwango cha kuharibika kwa ujauzito ama kujifungua kabla ya wakati na kujifungua kwa watoto wenye uzito chini ya gramu 100 walikuwa asilimia 1.8 (wamama 3/163) miongoni mwa wamama waliotibiwa mara tu baada ya uchunguzi, na asilimia 10.1 (19/188) miongoni mwa wamama ambao hawakupata tiba. Kiwango cha watoto waliozaliwa wakiwa na uzito mzito mdogo chini ya 1000 gramu na watoto njiti kilikuwa ni mara tano zaidi miongoni mwa kundi la wamama ambao hawakupata tiba.
Kuzaliwa kwa watoto njiti na watoto wenye uzito mdogo kunaongeza hatari ya kufariki kwa watoto wachanga. Bila shaka orodha ya matatizo yanayowaathiri watoto wanaozaliwa wakiwa njiti ni kubwa zaidi. Inasikitisha kuona kwamba imechukua muda mrefu sana kugundua kuwa matatizo yanayoweza kuzuilika na kutibika mapema kama magonjwa ya kinywa na meno yalivyoaathiri afya ya mama na mtoto mtarajiwa.
Tunatumai kuwa wahudumu wa afya ya mama na mtoto, mama mjamzito pamoja na madaktari wa meno watashirikiana pamoja kuzuia hatari kama hizi katika siku za usoni.
Imetafsiriwa kutoka http://ezinearticles.com