Image

Athari za mtoto kuchelewa kulala usiku

Taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Uingereza BBC, Julai 8 kuhusu utafiti uliofanyika nchini Uingereza uliowahusisha watoto 11,000 wakifuatiliwa kuhusu ratiba zao za kulala na kupima uwezo wa bongo zao.

Watafiti hao walisema ya kwamba wale watoto waliolala baada ya saa tatu usiku na waliokuwa hawana ratiba maalumu walikuwa na alama za chini kwenye hisabati na uwezo wa kusoma.

Na vilevile waliripoti kuwa ni vigumu ubongo kujifunza vitu vipya kutokana na ukosefu wa usingizi. Walichukua watoto wa kati ya miaka 3, 5 na 7 wakifuatilia uwezo wao wa kujifunza ukilinganisha na ratiba zao za kulala. Ratiba ilikuwa mbaya zaidi kwa watoto wa miaka 3. Na mpaka wanapofika miaka saba huwa na ratiba inayoeleweka kati ya saa moja na nusu usiku na saa mbili na nusu usiku.

Waliokuwa na ratiba nzuri ya kueleweka walifanya vizuri zaidi katika hisabati na kuwa na uwezo mkubwa  wa kusoma ukilinganisha na wenzao wasio na ratiba ya kueleweka na waliokuwa wanachelewa kulala .

Kuhusu kupungua uwezo wa ubongo athari zilionekana zaidi kwa wasichana ukilinganisha na wavulana. Utafiti huu uliofanywa na Prof. Amanda Sacker wa chuo kikuu cha London alisema kuwa vilevile mazingira mabaya ya familia zetu huweza kupelekea hali hii na aliijumuisha katika sababu za kupunguza uwezo wa ubongo.

Kitu Muhimu cha kuzingatia ni watoto kulala mapema na kumbuka bado hujachelewa,  ni vizuri kumuwekea ratiba nzuri ya kulala mtoto, na hakukuwa na ushahidi wa matokeo kuwa mazuri mtoto akilala kabla ya saa moja na nusu.

Kwa ujumla ili mtoto afanye  vizuri darasani ni vema apate usingizi mnono usiku.

Source: http://www.bbc.co.uk/news/health-23223751

Imesomwa mara 26546 Imehaririwa Jumatatu, 24 Julai 2017 11:46
Dr.Mayala

Dr.Henry A Mayala ni daktari bingwa Wa Tiba ya moyo katika taasisi ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI), ambaye kwasasa anasomea shahada ya uzamivu (PhD) ya Tiba ya Moyo katika Chuo Kikuu cha Tongji  nchini China.

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.