Tatizo la pingamizi la upumuaji usingizini huathiri zaidi wanaume kuliko wanawake.
Watu gani wako kwenye hatari ya tatizo hili?
• Unene uliopitiliza (Obesity)
• Shinikizo la damu (Hypertension)
• Moyo kushindwa kufanya kazi vizuri (Congestive Cardiac Failure)
• Matatizo katika mishipa ya damu ya moyo (Coronary Heart Disease)
• Unyongovu (Depression)
• Magonjwa sugu katika mfumo wa upumuaji (Chronic Obstructive Pulmonary Disease)
• Unywaji pombe kupita kiasi
• Uvutaji sigara kupita kiasi na matumizi ya madawa ya kulevya (ilicit narcotics)
• Historia ya mwana familia kuwa na tatizo hili.
• Watumiaji wa dawa zifuatazo: Barbiturates, Benzodiazepines, Ethanol,hypertensive and diabetic treatment----kwa kifupi dawa za usingizi, shinikizo la damu na kisukari
Dalili na Viashiria
• Kula zaidi kipindi cha mchana
• Kukoroma
• Ushuhuda wa mwenzi wako – wakati wa pingamizi la upumuaji au mitweto
• Kukosa usingizi kipindi cha usiku
• Uchovu
• Kuamka usiku kwenda kukojoa mara kwa mara
Vipimo Vya Uchunguzi
• Polysomnogram
• Actigraphy
Matibabu
Muendelezo chanya wa shinikizo katika mfumo wa hewa
Matibabu ya matatizo yanayoweza kupelekea kupata tatizo hili mfano kupunguza uzito kwa wale wenye uzito uliopitiliza, kutibu shinikizo la damu, kupunguza unywaji wa pombe na uvutaji sigara.