- Ostium secundum ASD
- Patent foramen ovale
- Otium primum ASD
- Sinus venosus ASD
- Common or single atrium
- Mixed ASD
Aina ya kwanza yaani Ostium secundum inaongoza kwa hutokea mara kwa mara, na huchangia kati ya asilimia 6 hadi 10 ya magonjwa yote ya moyo ya kuzaliwa nayo. Mtatatizo haya hutokana na uwazi wa tundu (foramen ovale) kuwa mkubwa, na kutokukua vema kwa kuta inayotenganisha (septum secundum). Hata hivyo karibu asilimia 70 ya watu wenye tatizo hili huweza kufikisha miaka 40 ndipo dalili huanza kujitokeza.
Dalili za tundu katika kuta za juu za moyo
- Kupumua kwa shida hasa wakati wa mazoezi
- Maambukizi ya mara kwa mara ya mfumo wa hewa kwa watoto
- Kuhisi mapigo ya moyo yanaenda haraka
- Uchovu
- Kujaa Miguu au kuvimba tumbo
- Ngozi kuwa ya bluu
Tundu kwenye kuta za juu za moyo
Madhara ya kuwepo kwa tundu kwenye kuta za juu za moyo
- Shinikizo la damu la mapafu (Pulmonary hypertension)
- Eisemnenger syndrome ni hali inayotokea pale ambapo uelekeo wa mkondo wa damu kutoka upande wa kushoto wa moyo kwenda upande wa kulia kupitia kwenye tundu zilizo kwenye kuta zinazotenganisha chemba za moyo huongeza mtiririko wa damu katika mishipa ya mapafu na kusababisha ongezeko la shinikizo la damu katika mapafu, hali ambayo hupelekea kuongezeka pia kwa shinikizo la damu katika upande wa kulia wa moyo, na hivyo kusababisha kubadilika kwa uelekeo wa damu kutoka upande wa kulia kwenda kushoto.
- Upande wa kulia wa moyo kushindwa kufanya kazi vizuri
- Hatari ya kupata kiharusi
Wanawake wajawazito wenye tundu katika kuta za juu za moyo (ASD) huweza kuvumilia hali hii na kuendelea na ujauzito bila matatizo yoyote lakini kwa wale ambao wameshapata madhara hali huwa wako katika hatari ya kupata madhara zaidi katika ujauzito hivyo, kwa wale ambao wameshapata madhara hushauriwa kuto shika mimba kwasababu huweza kuhatarisha maisha yao.
Vipimo
- Chest x-ray
- Echocardiogram – ni kipimo ambacho huweza kuonyesha tatizo, hasa tundu liko wapi.
- ECG
- Cardiac catheterization- hutumika kama kipimo na njia ya matibabu vilevile
- MRI
- Pulse oximetry- hutumika kuangalia kama damu yenye oksijeni inachanganyika na ile isiyo nayo
Matibabu
Matibabu ya awali ni ya kupunguza dalili ambayo huhusisha dawa zifuatazo
- Beta blocker-lopressor, inderal
- Cardiac glycoside- digoxin
Matatibu ya kutatua tatizo ni kati ya moja wapo ya njia hizi
- Upasuaji (open heart surgery) ili kuziba tundu na huweza kufanyiwa kwa watoto kati miaka 2 hadi 4
- Transcatheter approach –hapa mrija kitaalamu catheter upitishwa kwenye mshipa wa damu wa femoral hadi kwenye moyo na huwa na patch ambayo hubandikwa katika tundu na kurekebisha tatizo.