Image

Ufahamu ugonjwa wa Homa Ya Dengue

Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi viitavyo Dengue vinavyosambazwa na mbu aina ya Aedes . Mbu huyu anayeambukiza homa ya dengue hupendelea kuishi karibu na makazi ya watu na huweza kuuma binadamu mchana na usiku. Ugonjwa huu huathiri sana nchi za tropiko kama Amerika ya kusini na Africa. Ni moja kati ya homa kali inayodhoofisha na  kuambatana na maumivu makali. Kwa sasa, hakuna kinga ya homa ya dengue, njia pekee ya kuepuka ugonjwa huu ni kuzuia kuumwa na mbu anayesambaza homa ya dengue.

Je ni wapi homa hii upatikana zaidi duniani?

•India

•China

•Visiwa vya pasifiki

•Mexico

•Afrika

Dalili za homa ya dengue

•Homa kali ya ghafla

•Maumivu makali ya kichwa

•Macho kuuma

•Maumivu ya viungo

•Kichefuchefu

•Kutapika

•Vipele ambavyo hutokea siku nne baada ya homa kuanza

•Kutoka damu puani, kwenye fizi na kuchubuka kirahisi

Mara nyingi dalili huwa sio kali na wengi hudhania ni homa ya mafua au maambikizi mengine ya virusi. Dalili hizi huanza kutokea baada ya wiki mbili, lakini kwa wengi huchukua wiki moja ya kwanza na tayari utaanza kuona dalili za dengue.

Matatizo ambayo yanaweza kutokea baada ya maambukizi ya homa hii ni

•Homa kali zaidi

•Kuharibiwa kwa tezi na mishipa ya damu

•Kutokwa na damu zaidi puani na kwenye fizi

•Ini kuwa kubwa

•Na huweza kupelekea kifo

Vipimo

•Damu huchukuliwa na kuangalia virusi vya dengue au

• Kingamwili dhidi ya virusi hizi

Matibabu

Mpaka sasa hamna dawa kwa ajili ya ugonjwa huu ila  dawa za kupunguza homa na maumivu huweza kutumika kwa mfano:

•Paracetamol

•Pumzika vya kutosha

•Kunywa maji

•Nenda hospitali ukapate ushauri wa daktari

MUHIMU

Epuka dawa jamii ya aspirini maana huweza kusababisha damu iendelee kutoka. Na pia epuka kuendelea kuumwa na mbu anayesambaza dengue.

Kwa taarifa zaidi juu ya homa ya Dengue tafadhali tembelea http://www.denguevirusnet.com

Imesomwa mara 21359 Imehaririwa Jumanne, 05 Februari 2019 16:56
Dr.Mayala

Dr.Henry A Mayala ni daktari bingwa Wa Tiba ya moyo katika taasisi ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI), ambaye kwasasa anasomea shahada ya uzamivu (PhD) ya Tiba ya Moyo katika Chuo Kikuu cha Tongji  nchini China.

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.