Takribani asilimia 85 ya watu wenye harufu mbaya kinywani huwa na magonjwa ya kinywa na meno,Ikiwa harufu mbaya kinywani inasababishwa na magonjwa kinywani, dawa za kusafisha kinywa (mouthwash) haziwezi kuondoa tatizo zaidi ya kulifunika kwa muda tu.
Hakuna sababu ya kuona haya kumwambia daktari wa meno kuhusu harufu mbaya kinywani inayokusumbua, kwa vile kumwambia na kujadili tatizo lako ni njia ya kuelekea kwenye tiba ya uhakika. Matumizi ya nyuzi-safishi (dental floss) kila siku, kusafisha meno na ulimi kwa mswaki walau mara mbili kwa siku yaweza kuondoa harufu mbaya kinywani kwa kiasi kikubwa.
Unaweza kusoma Mambo 10 ambayo daktari wako wa meno angependa ufahamu