Image

Kunyonyesha kuna faida nyingi sana kwa mtoto mchanga pia na kwa mama. Na mara nyingi hili huwa ni umamuzi wa mtu binafsi ila ushauri wa msisitizo unatolewa na chama cha madaktari wa watoto na chama cha madaktari wa magonjwa ya wakina mama vyote vya marekani.

Faida kwa Mtoto

  • Virutubisho vilivyomo kwenye maziwa ya mama ni muhimu kwa mtoto mchanga , maana maziwa ya mama huwa uwiano mzuri wa vitamin, protini, na mafuta mazuri na kumuwezesha mtoto kukuwa vizuri
  • Vilevile maziwa ya mama huwa na virutubisho vyenye uwezo wa kumkinga mtoto kupata magonjwa kitaalamu antibodies, ambavyo humkinga mtoto mchanga dhidi ya vimelea (bakteria na virusi)
  • Maziwa ya mama hupunguza uwezekano wa mtoto mchanga kupata pumu au aleji
  • Na vilevile watoto wakinyonyeshwa kwa miezi sita mfululizo bila kuchanganyiwa na vyakula vingine hupunguza hatari ya kupata maambukizi ya masikio, mfumo wa hewa na magonjwa ya kuharisha
  • Kuna tafiti ambazo zinaonyesha maziwa ya mama yanaongeza upeo wa kufikiri wa mtoto atakapo kua
  • Vile vile kunyonyesha huongeza ukaribu wa mama na mtoto (bonding), na kuongeza mapenzi kati ya mama na mtoto.
  • Faida kwa mama

    • Husaidia kupunguza uzito kwa mama hasa baada ya kujifungua
    • Husaidia kutolewa kwa kichochezi Oxytocin ambacho husaidia kurudisha mfuko wa kizazi katika size yake ya zamani kabla ya ujauzito
    • Husaidia kupunguza hatari ya saratani za matiti na ovary, pia hupunguza hatari za matatizo ya mifupa
    • Husaidia kuwa karibu na mtoto (bonding)

     

     

    Imesomwa mara 6129 Imehaririwa Ijumaa, 22 Machi 2019 08:15
    Dr.Mayala

    Dr.Henry A Mayala ni daktari bingwa Wa Tiba ya moyo katika taasisi ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI), ambaye kwasasa anasomea shahada ya uzamivu (PhD) ya Tiba ya Moyo katika Chuo Kikuu cha Tongji  nchini China.

    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.