Image

Ni pale ambapo kunakuwa na mkusanyiko wa maji kati ya kuta mbili zinazozunguka  mapafu. Kujaa huku kwa maji husababisha mgonjwa kupata shida ya kupumua vizuri.


Je mapafu kujaa maji husababishwa na nini?

Sababu za Mapafu kujaa maji zinaweza kuelezewa kutokana na aina ya maji yaliyojaa:

  • Transudate – hapa maji huliki kutoka kwenye mishipa ya damu na kuingia kwenye mapafu mfano kwenye magonjwa yafuatayo:
  • Moyo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi (congestive cardiac failure)
  • Ini kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi (liver failure)
  • Figo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi (renal failure)
  • Exudate – hapa maji hujaa kutokana na kuta zinazonguka mapafu kitaalamu pleura zinapovimba au kutokana na magonjwa ya mapafu mfano:
  • Kansa ya pafu au ya titi
  • Lymphoma
  • Kifua kikuu
  • Vichomi
  • SLE
  • Figo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi 
  • Asbestosis
  • Majipu ndani tumbo


Dalili:

  • Kusindwa kuhema vizuri
  • Maumivu ya kifua
  • Kifua kikuu- Jasho jingi kutoka kipindi cha usiku, kukohoa damu, kupungua uzito 
  • Vichomi- homa , kukohoa, makohozi yenye rangi

Vipimo:

  • Picha ya kifua kikuu (x-ray)
  • Ultrasound ya kifua
  • CT-scan
  • Thoracentesis 
  • Vipimo vya damu

 

Matibabu:

Kwasababu ya kusababisha matatizo ya kupumua inabidi kuanza na ABC za kuokoa maisha, angalia mfumo wa hewa na kadhalika . tibu magonjwa yanayosababisha kupunguza maji kwenye mapafu kunaweza kutumika kwa ajili ya kipimo au matibabu ya kumpa nafuu mgonjwa

 

Imesomwa mara 26437 Imehaririwa Ijumaa, 01 Februari 2019 18:25
Dr.Mayala

Dr.Henry A Mayala ni daktari bingwa Wa Tiba ya moyo katika taasisi ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI), ambaye kwasasa anasomea shahada ya uzamivu (PhD) ya Tiba ya Moyo katika Chuo Kikuu cha Tongji  nchini China.

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.