Ni tatizo ambalo huathiri wote wanaume na wanawake, vilevile watu wa rika yote kwa ujumla. Tatizo hili husababishwa na mpasuko au mchaniko katika eneo la mwisho la mfereji wa haja kubwa.
Nini husababisha mwatuko wa mfereji wa haja kubwa?
Aina yoyote ya ajali katika mfereji wa haja kubwa husababisha mwatuko kama ifuatavyo:
- Kupata choo kingi na kigumu kwa muda mrefu
- Tatizo sugu la kuharisha
- Kuvimba kwa eneo la mfereji wa haja kubwa (inflammation)
Sababu nyinginezo ni kama zifuatazo
- Ngono ya njia ya haja kubwa
- Kansa
- Virusi vya ukimwi
- Kaswende
- Kifua kikuu
Watu gani wanaweza kupata tatizo hili?
- Watoto chini ya mwaka mmoja (infants)
- Umri mkubwa- kwasababu kuna upungufu wa ugavi wa damu katika mfereji wa njia ya haja kubwa
- Kupata choo kigumu kwa muda
- Wanawake wakati wa kujifungua
- Crohn’s disease
Dalili
- Maumivu mara baada ya haja kubwa
- Damu kwenye kinyesi na huonekana kwenye karatasi ya chooni (toilet paper)
- Maumivu huweza kuwa makali mpaka kumfanya mtu ajizuie kwenda msalani
- Kuwashwa
Vipimo na uchunguzi
- Sigmoidocopy
- Colonoscopy
Matibabu
Huweza kutibiwa kwa dawa katika hatua za awali
- Dawa za kulainisha choo
- Sitz bath
- Cream za kupaka (Anusol, zinc oxide)
- Nitroglycerin
- Botox
- Calcium channel blockers (nifedipine and diltiazem)
Kama tatizo hili limekuwa sugu na halitibiki kwa tiba nyingine, basi Upasuaji ndio huwa tiba mwafaka
- Partial lateral internal sphicterotomy
- Anal dilation
Jinsi ya kuzuia mwatuko wa mfereji wa haja kubwa
- Vyakula vya kulainisha choo - matunda na mbogamboga
- Kunywa maji mara kwa mara
- Na fanya mazoezi