Image

Kujiua kwa Vijana: Changamoto, Sababu, na Ufumbuzi.  

 

Kujiua kwa vijana ni tatizo kubwa la afya ya akili linaloendelea kuongezeka duniani kote, ikiwa ni pamoja na Tanzania. Takwimu za mwaka 2019 zinaonyesha kuwa kujiua ilikuwa sababu ya nne ya vifo kwa watu wenye umri wa miaka 15 hadi 29 duniani kote, ambapo vifo vingi vilitokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati. Tafiti za ARISE Network katika nchi sita za Afrika zilionyesha kuwa katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, kiwango cha mawazo ya kujiua, mipango, na majaribio ya kujiua kilikuwa kati ya 1.2% na 12.4%.Aidha, utafiti wa Africa Academy for Public Health mkoani Tanga, Tanzania, ulionyesha kuwa vijana 2 kati ya 100 walishawahi kujaribu kujiua, huku wale waliokuwa nje ya mfumo wa shule wakiwa na hatari kubwa zaidi ikilinganishwa na wenzao waliokuwa shuleni.

Ni muhimu kuelewa sababu, dalili, na hatua za kuzuia ili kusaidia vijana wanaopitia changamoto za maisha na kuzuia matukio ya kujiua.

 Sababu Zinazochangia Kujiua kwa Vijana

  •  Shinikizo kutoka kwenye jamii inayowazunguka na shinikizo la Kimaisha: Vijana wanakabiliwa na shinikizo kubwa katika mambo kama vileushindani wa juu katika masomo , kukatishwa tamaa na wazazi, au kushindwa kufikia matarajio yaliyowekwa na jamii kunaweza kuwasababisha kujihisi kukosa thamani.
  • Matatizo ya Afya ya Akili: Magonjwa ya akili kama vile sonona, wasiwasi ulioptiliza, na ugonjwa wa kama vile bipolar/mwezi mchanga yanaweza kuongeza hatari ya kujiua.
  • Matatizo ya Mahusiano: Migogoro ya kifamilia, urafiki, au mapenzi inaweza kuathiri sana afya ya akili ya kijana.
  • Unyanyapaa na Upweke: Unyanyapaa unaohusishwa na afya ya akili unaweza kuzuia vijana kutafuta msaada, na upweke unaweza kuzidisha hisia za huzuni na kutokuwa na tumaini na kupelekea mawazo ya kujiua na hata kuchukua hatua hiyo ya kujiua
  • Utumiaji wa Dawa za Kulevya na vileo kupita kiasi : Matumizi ya dawa za kulevya na pombe yanaweza kuongeza hatari ya kujiua kwa vijana.
  • Udhalilishaji wa Mtandaoni: udhalilishaji mtandaoni unaweza kuwa na athari kubwa kwa afya ya akili ya vijana na kupelekea kujiua

 Dalili za Hatari za Kujiua

  •  Mabadiliko ya Tabia: Mabadiliko ghafla katika tabia, kama vile kujitenga na marafiki na familia, kupoteza hamu ya shughuli ambazo alikua anafurahia kufanya mwanzoni, au mabadiliko katika tabia ya kulala au kula.
  • Mawazo ya Kifo: Kuzungumza mara kwa mara kuhusu kifo, kujiua, au kutokuwa na
  • Kupoteza Haamu ya Kufanya Maamuzi: Kushindwa kufanya maamuzi ya kila siku au kutojali matokeo.
  • Kuongezeka kwa Tabia hatarishi: Kujihusisha katika tabia za hatari kama vile kuendesha gari kwa mwendo wa kasi kupitiliza ,Kujiumiza kimakusudi na kadhalika

 Kuzuia Kujiua kwa Vijana

  • Kutoa Elimu: Elimu kuhusu afya ya akili ni muhimu katika kupunguza unyanyapaa na kuhamasisha kutafuta msaada.
  • Kuimarisha mahusiano na familia, marafiki, na jamii kunaweza kutoa msaada wa
  • Kutafuta Msaada wa Kitaalamu: Huduma za afya ya akili, kama vile tiba ya na dawa, zinaweza kusaidia kupunguza dalili za magonjwa ya akili.
  • Kuhamasisha Mazungumzo ya Wazi: Kuhamasisha mazungumzo ya wazi kuhusu afya ya akili na hisia kunaweza kusaidia vijana kujisikia vizuri zaidi.
  • Kupunguza Upatikanaji wa Njia za Kujidhuru: Kupunguza upatikanaji wa silaha za moto na dawa za kulevya inaweza kupunguza hatari ya kujiua.
  • Kuimarisha Sera za Afya ya Akili: Serikali na taasisi za afya zinapaswa kuwekeza katika huduma za afya ya akili kwa vijana.

 Jukumu la Kijana

Kijana anapaswa kuelewa kuwa changamoto za maisha ni sehemu ya ukuaji. Kupitia mafunzo, mazungumzo na watu wanaowaamini, wanaweza kupata msaada wa kuondoa changamoto za kimaisha. Kujihusisha na vikundi vya kijamii vyenye usaidizi mzuri pia kunasaidia.

Jukumu la Wazazi na Jamii

Wazazi na wana jamii wanapaswa kuwa msaada kwa vijana kwa kuonyesha upendo, huruma, na kuelewa changamoto wanazopitia. Kuwapa nafasi ya kujieleza bila kuhukumiwa na kuhakikisha wanapata msaada wa kitaalamu pale inapohitajika ni njia muhimu ya kuzuia kujiua.

Ikiwa unajua mtu anayekabiliwa na mawazo ya kujiua, tafadhali tafuta msaada mara moja. Unaweza kuwasiliana na huduma ya dharura ya afya ya akili au kuzungumza na mtaalamu wa afya ya akili.Kumbuka, hauiko peke yako. Kuna msaada uliopo.

 

 

Imesomwa mara 305 Imehaririwa Jumanne, 28 Januari 2025 18:29
Dr. Hussen Mshunga

As a highly trained and experienced specialist in the field of psychology with a close decade of experience in the field. I am an expert in the early identification and intervention of neurodevelopmental challenges in Tanzania and the United States.

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.