Image

Dalili za ugonjwa wa Ukimwi na jinsi ya kujikinga

VVU/UKIMWI bado unaendelea kuwa janga katika jamii yote ya dunia ikiwa imeshasababisha vifo vya watu takribani millioni 33 mpaka sasa kulingana na taarifa ya WHO ya mwaka 2020.

Mpaka waka 2019 takribani ya watu million 38 walikuwa  wanaishi na maambukizi ya VVU, Tanzania pekee ni watu millioni 1.6 wanaoishi na maambukizi hayo kwa taarifa ya mwaka 2018 pekee.

Hivyo taaarifa hizi zinaonyesha umuhimu wa kupima, kujua dalili na kujikinga na maambukizi ya VVU.

Hebu zifahamu dalili za ugonjwa wa VVU/UKIMWI

Moja kati ya changamoto kubwa kuhusu ugonjwa huu ni kuwa mara nyingi mtu mwenye maambukizi hatoonyesha dalili zozote hadi hapo baadae ugonjwa utakapo fika hatua mbaya zaidi. Sambamba na hilo dalili zake nyingi za awali hazina uhusika wa moja kwa moja na ugonjwa huu maana zinaweza sababishwa na magonjwa mengine.( non specific symptoms).

Na dalili hizi hutegemeana sana na hatua (stage) ya ugonjwa

Pindi mtu anapokuwa amepata maambukizi uanza na dalili zifuatizo katiki wiki chache za mwanzo (2-4) au kutokuwa na dalili kabisa. Dalili za awali na kama zifuatazo

  • Homa
  • Kichwa kuuma
  • Miwasho au vipele
  • Madonda ya koo (sore throat)
  • Maumivu ya misuli na kuchoka
  • Kuvimba matezi
  • Kutoka jasho jingi
  • Kukosa hamu ya kula
  • kuharisha N.K

ukiona una dalili moja wapo kati ya hizi na umeshiriki tabia yoyote hatarishi ya ugonjwa wa VVU/UKIMWI unashauriwa ukifike kituo cha afya kwaajili ya kipimo cha VVU na kupata ushauri.

Kama nilivyoandika hapo awali unaweza usiwe na dalili yoyote hadi hapo baadae ambapo kinga yako imedhohofika kutokana na virusi hivi kushambulia chemechembe nyeupe dama (CD4) zinazo saidia kinga ya mwili.

Dalili zifuatazo na magongwa nyemelezi hutokea pindi unapo kuwa na usugu wa ugonjwa huu na kinga kushuka.

  • Utando mweupe mdomoni
  • Fungusi ukeni
  • Malengelenge mdomoni na sehemu za siri (herpes simplex)
  • Mkanda wa jeshi
  • Vipele vyeusi mwili mzima (pruritic Papura Eruptions)
  • Saratani mfano saratani ya shingo ya uzazi, saratani za ngozi (karposi sarcoma)
  • Kifua kikuu
  • Kupungua uzito
  • Fangasi ya uti wa mgongo (criptococcal mengitis)
  • Upungufu wa damu
  • Gonjwa la akili utokanao na VVU/UKIMWI (HIV encephalopathy)
  • Gonjwa la figo litokanalo na UKIMWI n.k

Ugojwa huu haina tiba wala chanjo lakini habari njema ni kwamba unaEPUKIKA! Aidha kabla ya kujua jinsi ya kujikinga ni muhimu kufahamu kwa sehemu jinsi ugongwa huu unavyosambaa.

Ugonjwa huu huambukizwa kwa kubadilishana majimaji na mtu aliyeathirika kama vile damu, maziwa, shahawa au majimaji kutoka kwenye uke. Pia huambukizwa kutoka kwa mama kuja kwa mtoto wakati wa ujauzito,kujifungua na kunyonyesha.

Zifuatazo na njia mbali mbali za kujikinga na VVU/UKIMWI.

Ile kujinga a ugonjwa wa VVU/UKIMWI ni muhimu kuondoa kabisa au kupunguza tabia hatarishi kwako.

Matumizi ya kondomu za kike na kiume

Ni vema kutumia kondomu pindi unapojamiana na mtu usiye jua hali yake au mwenye maambukizi ya VVU. Tafiti zinaonyesha kondomu huzuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi kwa Zaidi ya asilimia 85. Zingatia uvaaji sahihi wa kondomu.

Kuzuia maambukizi ya mama kwenda wa mtoto

Mtoto wa mama mwenye maambukizi huweza kupata maambukizi wakati wa ujauzito wakati wa kujifungua na kunyonyesha. Tafiti zinaonyesha kiwango cha maambukizi huanzia asilimia 15 hadi 45 bila kufanya harakati ya kuzuia maambukizi hayo.

Ili kuzua maambukizi mama mjamzito anapaswa kujua hali yake kabla na pindi unapokuwa mjamzito, na kama umeathirika anapaswa kuanza dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI mara. Pindi unapojifungua, mtoto huanzishiwa dawa maalum ya kumkinga na maambukizi kwa miezi sita huku akifanya vipimo kuthibitisha kama amepata maambukizi tiyari. Taarifa hizi na huduma za vipimo na madawa hutolea kliniki hivyo kuhudhuria kliniki ni muhimu sana.

Tohara kwa wanaume

Tohara imeonyesha kusaidia kupunguza maambukizi ya VVU kwa wanaume kwa asilimia 60 na sio kuzuia kama ilivyodhana potofu ya watu wengi. Hivyo hakikisha kwa hiari unafanyiwa tohara mapema ili kupumguza hatari ya kupata maambubikizi.

Kutokuchangia vitu vyenye uncha kali kama sindano, viwembe n.k. Kundi maalum hapa ni waathirika wa madawa ya kulevya maana hujidunga madawa kwa kuchangia mabomba ya sindano. Kundi hili ni muhimu kupata matibabu kuondoa ulevi wa madawa ili kuwalinda na maambukizi.

Uaminifu hii pia jia ya kujikinga na maambukizi kwa kuwa mwaminifu kwa mpenzi mmoja hasa kwa wanandoa

Matumizi ya madawa ya kufubaza makali virusi vya UKIMWI- tafiti zinaonyesha kuwa mtu anayetumia madawa haya anakuwa hana huwezo mkubwa wa kuambukiza ukilinganisha na ambae hatumii kabisa au anayetumia kwa kusuasua.

Kinga baada ya kuwemo hatarini (post exposure prophylaxisis PEP)

Hizi na dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWIi zinazotolea kama kinga ndani ya masaa 72 pindi mtu anapokuwemo kwenye hatari ya maambukizi. Dawa hizi hutolewa kwa muda wa siku 28 pamoja na ushauri nasaa na vipimo.

 

USHAURI na Mazingatio

Pamoja na kujua dalili na jinsi ya kujinga na VVU/UKIMWI ni muhimu sana kujenga tabia ya kupima na kujua afya yako mara kwa mara na kuepuka tabia hatarishi. Usiogope maana hata ukigundulika na ugonjwa huu huo sio mwisho wa maisha. Sasa waweza ishi na kuwa na furaha hata kama umeathirika.

 

 

 

 

Imesomwa mara 20515 Imehaririwa Jumapili, 08 Agosti 2021 22:22
TanzMED Admin

TanzMED ni mjumuiko wa wataalamu wa fani mbalimbali za Afya na IT wa kitanzania ambao wamejitoa katika kuhakikisha kuwa jamii ya kitanzania na Afrika kwa ujumla inafaidika kwa kupata habari na ushauri juu ya masuala ya afya yanayozunguka jamii hizo.

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.